Loading...

VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA

Loading...
VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA
link : VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA

soma pia


VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba Viongozi wa Jumuiya na Taasisi zote za kidini nchini wahakikishe wanawapiga vita watu wote wanaopanga na kutaka kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa sababu watakwamisha maenendeleo. 

Amesema Serikali inaelewa kwamba dini ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya maendeleo ya ustaarabu wa mwanadamu kwani inatoa elimu ya maadili mema yenye kuwafanya waumini waepukane na maovu mbalimbali.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Oktoka 01, 2017) wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa 48 wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya uliofanyika katika eneo la Kitonga kata ya Msongola wilayani Ilala, Dar es Salaam. Amesema kila Mtanzania anatakiwa ahakikishe anadhibiti matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika.”Tanzania ni nchi salama na yenye utulivu, hivyo ni lazima wote tushirikiane kuitunza.”

“Napenda niwahakikishieni kuwa Serikali inaunga mkono juhudi za Jumuiya  za kidini katika kupiga vita maovu ya kila aina; mathalan utumiaji wa dawa za kulevya, wizi, rushwa, uzinzi ambao husababisha madhara mengi ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.” Amesema iwapo dini zetu zitatumika vizuri tutaweza kwa haraka sana kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la ‘Hapa kazi tu’ kwani kila mtu ataepuka uzembe na kuwajibika ipasavyo.

Waziri Mkuu amesema ana imani kwamba jumuiya hiyo kama zilivyo taasisi zingine za kidini itaendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii yetu kwa kuwapatia waumini wao na wananchi kwa ujumla elimu na maarifa ya kuboresha tabia zao na maadili yao kiroho.Amesema amani na utulivu uliopo nchini unatokana na mambo mengi ikiwemo na wananchi kupata ustawi, kuweza kufanya shughuli zao vizuri na kuwa na imani na Serikali yao, ambayo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi hususan wanyonge wanapata faraja ndani ya nchi yao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na kiongozi na mbashiri mkuu  wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,Tahir Mahmood, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar  es salaam Oktoba 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waumini wa Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, kabla ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo huko Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kitabu kutoka kwa Katibu wa Malezi Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania, Mahmood Hamsin, baada ya kufungua mkutano mkuu wa 48 wa jumuiya hiyo Mbande, Temeke, Jijini Dar es salaam Oktoba 1, 2017. (kulia) ni. kiongozi na mbashiri mkuu wa  Jumuiya ya waislamu wa Ahmadiya Tanzania,Tahir Mahmood. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 


Hivyo makala VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA

yaani makala yote VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/viongozi-wa-dini-wawapinge-wanaotaka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VIONGOZI WA DINI WAWAPINGE WANAOTAKA KUVURUGA AMANI-MAJALIWA"

Post a Comment

Loading...