Loading...
title : WATAKIWA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI
link : WATAKIWA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI
WATAKIWA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI
Ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajili nchini, wanafunzi wametakiwa kuyapenda masomo ya sayansi na hesabu ambayo yatawajengea uwezo wa kupata ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda.
Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, mhandisi Nada Narya aliyasema hayo kwenye mahafali ya pili ya darasa la saba na ya nane ya kumalizika elimu ya awali ya shule hiyo.
Mhandisi Narya alisema shule hiyo imewaanda ipasavyo wanafunzi wa shule hiyo kupenda masomo ya sayansi na hesabu ili kukabiliana na tatizo la ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hivyo wanafunzi wengine nchini wapende masomo hayo.
Alisema hivi sasa soko la ajira ni dogo na ili kuondokana na hali hiyo inawapasa wanafunzi kuyapenda masomo sayansi na hesabu kwa lengo la kujiandaa kwa nguvu zote katika kuhakikisha wanajipanga ipasavyo hivi sasa ili baadae wachangamkia fursa ya ajili kupitia Tanzania ya viwanda.
"Sisi kama Deira tumeanza kuwaandaa wanafunzi wetu wapende masomo ya sayansi na hesabu ili baadaye waweze kuendesha maisha yao kwenye soko la ajira kwani wataalamu mbalimbali watatokea hapa shuleni kwetu," alisema mhandisi Narya.
Ofisa elimu msingi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, Doroth Mwandila akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium Vannesa Nada, cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (kushoto) ni Mkurugenzi wa shule hiyo mhandisi Nada Narya.
Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, wakionyesha mchezo wa kareti wakati wa mahafali yao yaliyofanyika shuleni kwao.
Hivyo makala WATAKIWA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI
yaani makala yote WATAKIWA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATAKIWA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/watakiwa-kuyapenda-masomo-ya-sayansi.html
0 Response to "WATAKIWA KUYAPENDA MASOMO YA SAYANSI"
Post a Comment