Loading...
title : DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA
link : DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA
DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiongea na wananchi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na nguvu za wananchi, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitokea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua kimaendeleo. PICHA NA KAJUNASON/MMG – HANDENI, TANGA.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akimsaidia Diwani wa Kata ya Kwamgwe, Sharifa Abebe alipokuwa akitoa machozi ya shukrani kwa shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kuweza kushirikiana na wananchi kuwajengea jengo la zahanati lililoweza kugharimu shilingi milioni 190 ambapo wao World Vision Tanzania waliweza kutoa Milioni 100 na wao wananchi waliweza kujitoa kwa nguvu zao kwa thamani ya milioni 90. Hafla hiyo ilifanyika katika Kata ya Kwamgwe ambapo ndipo jengo hilo lilipojegwa.
Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania, Humphrey Bernard akisoma risala ya mradi wa ujenzi wa zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwamgwe ambapo aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha ujenzi wa jengo la zahanati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni, William Makufwe akitoa ufafanuzi jinsi wananchi walivyoweza kujitoa ujenzi wa zahanati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni, William Makufwe akitoa ufafanuzi jinsi wananchi walivyoweza kujitoa ujenzi wa zahanati.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Dokta Credianus akitoa nasaha zake kwa wananchi wa Handeni waweze kujua umuhimu wa kuwekeza katika afya.
Jengo la zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwangwe, Wilayani Handeni.
Wakati huo huo, mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akipokea zawadi ya kuku kutoka wa mwenyekiti wa kitongoji cha Migombani, Michungwani-Segera Bi. Amina Njama ambaye amekuwa msitari wa mbele katika uhamasishaji wa kukusanya matofali ili yaweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa na zahanati.
Jengo la zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwangwe, Wilayani Handeni.
Wakati huo huo, mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akipokea zawadi ya kuku kutoka wa mwenyekiti wa kitongoji cha Migombani, Michungwani-Segera Bi. Amina Njama ambaye amekuwa msitari wa mbele katika uhamasishaji wa kukusanya matofali ili yaweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa na zahanati.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewataka wananchi wa Kata ya Kwamgwe kuendelea kujitoa kikamilifu katika kuchangia shughuli za kijamii ili kuendana na kasi ya rais Dkt. John Magufuli katika kuleta maendeleo endelevu.
Akizungumza na wakazi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitolea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua.
“Nawaomba ndugu zangu, sisi wote ni wanaKwamngwe, lazima tuamue kuchangua mambo muhimu matatu, kutambaa, kutembea au kukimbia. Jambo la msingi ni lazima tuwe katika mwendo, tuendelee kujitoa tuzidi kuleta maendeleo kijijini kwetu,” alisema Gondwe.
Awali akikabidhi mradi huo wa zahanati hiyo, Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP, Humphrey Bernard aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha ujenzi wa jengo la zahanati.
Wakati huo huo, Mkuu wa wilaya Handeni aliweza kutembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Michungwani, Segera ambapo ujenzi wake unaanza hivi karibuni kwa nguvu za wananchi kupitia kampeni ya mkuu huyo ya kuongeza zahanati na madarasa.
Hivyo makala DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA
yaani makala yote DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/dc-gondwe-awataka-wananchi-wasichoke_23.html
0 Response to "DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA"
Post a Comment