Loading...
title : DKT MWANJELWA: SERIKALI KUFANIKISHA UWEPO WA SOKO LA BIDHAA (COMMUNITY EXCHANGE)
link : DKT MWANJELWA: SERIKALI KUFANIKISHA UWEPO WA SOKO LA BIDHAA (COMMUNITY EXCHANGE)
DKT MWANJELWA: SERIKALI KUFANIKISHA UWEPO WA SOKO LA BIDHAA (COMMUNITY EXCHANGE)
Na Mathias Canal, Dodoma.
Serikali inaendelea na mchakato wa kufanikisha uwepo wa Mfumo wa soko la bidhaa (Commodity Exchange) ambapo miongoni mwa kazi za Mfumo huo utalenga kupunguza gharama za uendeshaji wa masoko ya mazao yote ya chakula na biashara ili kuwawezesha wakulima kupata bei nzuri na yenye tija.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa Bungeni Mjini Dodoma Wakati akijibu swali la Mbunge wa Lulindi Mkoani Mtwara Mhe JEROME DISMAS BWANAUSI aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanzisha mfumo wa “Commodity Exchange” ili kuwasaidia wananchi wanaolima Korosho kupata bei nzuri katika misimu husika.
Mhe Naibu Waziri alisema kuwa Maandalizi ya Soko la Bidhaa (Commodity Exchange) yalianza tangu mwaka 2011 kwa lengo la kufanya biashara ya mazao kuwa ya wazi na yenye ushindani kulingana na nguvu ya soko.
Mhe Mwanjelwa alizitaja hatua ambazo zimechukuliwa na serikali mpaka hivi sasa kuwa ni pamoja na kupitishwa kwa Waraka wa Soko hilo, Kuundwa kwa Bodi ya Soko, kutungwa kwa Sheria ya mwaka 2015 ya Soko la Bidhaa pamoja na kanuni zake, Kufanya uzinduzi wa kuanzisha Soko hilo, Kutoa mafunzo kwa Madalali watakaoendesha soko hilo na Kutoa mafunzo kwa baadhi ya viongozi wa Serikali na Sekta Binafsi ili kujenga uelewa wa pamoja.
Hivyo makala DKT MWANJELWA: SERIKALI KUFANIKISHA UWEPO WA SOKO LA BIDHAA (COMMUNITY EXCHANGE)
yaani makala yote DKT MWANJELWA: SERIKALI KUFANIKISHA UWEPO WA SOKO LA BIDHAA (COMMUNITY EXCHANGE) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT MWANJELWA: SERIKALI KUFANIKISHA UWEPO WA SOKO LA BIDHAA (COMMUNITY EXCHANGE) mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/dkt-mwanjelwa-serikali-kufanikisha.html
0 Response to "DKT MWANJELWA: SERIKALI KUFANIKISHA UWEPO WA SOKO LA BIDHAA (COMMUNITY EXCHANGE)"
Post a Comment