Loading...
title : MCT KUINGILIA KATI UHURU WA WANAHABARI
link : MCT KUINGILIA KATI UHURU WA WANAHABARI
MCT KUINGILIA KATI UHURU WA WANAHABARI
Na Noel Rukunuga.
Baraza la Habari Tanzania (MCT) limerahani matukio ya uvunjifu wa uhuru kwa waandishi wa habari ambayo ynaendelea kutokea kutokana na matukio 30 yaliotokea kuhusu hapa nchini.
Kutokana na matukio hayo MCT itawafikisha mahakamani wote wanaowazuia, kuwanyanyasa na kuwapiga waandishi wa habari wawapo katika majukumu yao ya kazi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari jleo ijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kupinga Jinai Dhidi ya Wanahabari, yanayofanyika duniani kote na kwamba baraza linachukua hatua hiyo kutokana na vitendo hivyo kushamiri .“MCT haliridhishwi na mwenendo wa hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini . Inasisitiza kuwa haki ya kupata habari na uhuru wa kujieleza ni haki ya Kikatiba,” amesema Mukajanga.
Akitolea ukiikwaji wa haki hizo ni katika kipindi cha miezi sita iliyopita magazeti matano yemefungiwa ambayo ni Mseto, Mwanahalisi, Mawio, Tanzania Daima na Raia Mwema.
Amesema mbali na kufungiwa kwa vyombo hivyo, waandishi mbali mbali wamepata misukosuko wakati wakiwa kazini. Baadhi yao ni Halfani Lihundi wa ITV Arusha, ambaye aliwekwa kizuizini na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.
Mwingine ni Augusta Njonji wa Nipashe ambaye hivi karibuni aliandika habari za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na kukamatwa na kuhojiwa na polisi na baadae kuachiwa kwa dhamana.
Pia waandishi wa Mwananchi, Azam TV na Mtanzania huko Geita nao walipata msukosuko wakati wakiwa kazini kuripoti rabsha za wanafunzi wa Sekondari ya Geita hivi karibuni.
Matukio mengine amesema ni pamoja na waandishi Joel Maduka wa Storm FM na Vallence Robert wa Channel Ten kushambuliwa na polisi wakiwa kwenye msafara wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa huko Geita.
Wengine ni wapiga picha wa Kampuni ya The Guardian Ltd, Selean Mpochi na John Badi, ambao walinyang’anywa kamera zao wakati wakifanya kazi zao katika mkutano wa Sheikh Ponda katika hotel ya Iris ya jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Amesema ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa waandishi wa habari amekuwa ni kwa serikali kupitia polisi, wakuu wa mikoa na wilaya.
Hivyo makala MCT KUINGILIA KATI UHURU WA WANAHABARI
yaani makala yote MCT KUINGILIA KATI UHURU WA WANAHABARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MCT KUINGILIA KATI UHURU WA WANAHABARI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mct-kuingilia-kati-uhuru-wa-wanahabari.html
0 Response to "MCT KUINGILIA KATI UHURU WA WANAHABARI"
Post a Comment