Loading...
title : NAIBU WAZIRI WA SHERIA WA CHINA KUTEMBELEA TANZANIA
link : NAIBU WAZIRI WA SHERIA WA CHINA KUTEMBELEA TANZANIA
NAIBU WAZIRI WA SHERIA WA CHINA KUTEMBELEA TANZANIA
Mwambawahabari
Naibu Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Watu China Mhe. Zhao Dacheng anatarajia kuwasili jijini Dar es salaaam leo kwa ziara ya siku nne nchini.
Naibu Waziri huyo wa Sheria wa China anakuja nchini kufuatia mwaliko wa Waziri wa Katiba na Sheria nchini Prof. Palamagamba Kabudi.
Mara baada ya kuwasili nchini Mhe. Dacheng atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi jijini Dar es salaaam ambapo pamoja na mambo mengine watazungumzia maeneo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na China.
Siku ya Alhamis Prof. Kabudi na mgeni wake mhe. Dacheng wanatarajia kutembelea Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na taasisi nyingine zinazojihusisha na masuala ya msaada wa kisheria.
Disemba Mosi Mhe. Dacheng atafanya ziara ya siku moja katika kisiwa cha Zanzibar ambako pia atakutana na Jaji Mkuu wa Tanzania mhe.Prof. Ibrahim Juma na viongozi wengine wa Zanzibar.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA SHERIA WA CHINA KUTEMBELEA TANZANIA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA SHERIA WA CHINA KUTEMBELEA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA SHERIA WA CHINA KUTEMBELEA TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/naibu-waziri-wa-sheria-wa-china.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA SHERIA WA CHINA KUTEMBELEA TANZANIA"
Post a Comment