Loading...
title : Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora
link : Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora
Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora
Na.WAMJW,Mtwara
Serikali inatarajia kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora wa kutoa huduma za afya ili mwananchi wajue kituo atakachoenda kina ubora gani wa huduma hivyo nchini
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akiongea na Viongozi na Watendaji wa afya wa Mkoa na Wilaya zake kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao kwa wilaya iliyofanya vizuri na vituo vya afya vilivyofanya vizuri wakati wa zoezi la tathimini ya kutoa nyota kwa vituo vya kutolea huduma za afya.
Dkt.Ndugulile alisema hivi sasa serikali inasisitiza kuweka ubora wa huduma za afya katika vituo vyote vya afya vya umma ili kukidhi ubora unaotakiwa wa kutoa huduma kwa wananchi”tunakwenda mbali zaidi usipokuwa na vigezo hospitali yako na kituo chako hutopewa leseni”
Hata hivyo amewataka wale wote waliopewa maelekezo ya nini wafanye basi viongozi wawajibike kwa kurekebisha changamoto zilizopo na wasingoje idara ya uhakiki ubora kutoka wizarani waje kukagua kwani Lengo liliowekwa na wizara ni kila kituo cha afya kupata nyota tatu hadi kufikia mwezi juni mwakani.
“Nyinyi wengine wote hamkustahili kupata cheti hata kimoja hapa,Mkoa wa Mtwara asilimia 3 za vituo vyenu vina nyota mbili na asilimia 51 vina nyota moja na zaidi ya nusu mna nyota 1 na asilimia 46 mna nyota sifuri hali ya utoa huduma bado”Nimetoka hapo zahanati ya Ziwani,kwakweli hapana,ubora wa kutoa huduma pale hapana wakati mpo mjini.
Naibu Waziri akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuibuka mshindi.Dkt.Ndugulile aliipongeza Wilaya hiyo kwa mpangilio mzuri wa utoaji huduma pamoja na utunzaji wa kumbukumbu kwenye stoo ya dawa katika kituo cha afya cha Mtambaswala ambacho kimeanza miezi miwili iliyopita lakini kimeonyesha ufanisi wa hali ya juu.
Picha ya pamoja mara baada ya Naibu Waziri kutoa ngao na vyeti kwa washindi kwa Mkoa wa Mtwara
Dkt.Ndugulile akisoma taarifa ya dawa katika Zahanati ya Ziwani iliyopo Manispaa ya Mtwara,ambapo Naibu Waziri huyo alichukizwa hali ya miundombinu na uwajibikaji wa Zahanati hiyo na kuwapa miezi miwili wawe wamefanya marekebisho kama walivyoelekezwa.
Mkuu wa Zahanati ya Shangani akipokea cheti kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya.
Hivyo makala Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora
yaani makala yote Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/serikali-kutoa-leseni-kwa-hospitali-na.html
0 Response to "Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora"
Post a Comment