Loading...
title : NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFANYA ZIARA TUNDURU,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA TAIFA
link : NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFANYA ZIARA TUNDURU,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA TAIFA
NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFANYA ZIARA TUNDURU,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA TAIFA
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Josephat Kandege amefanya ziara wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Katika ziara hiyo, aliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera ambae aliambatana na kamati yake ya Ulinzi na Usalama. Akiwa katika ziara hiyo Kadege alikagua vituo viwili vya Afya cha Matemanga na Mkasale.
Amesema lengo la ziara hiyo ilikuwa kuona utekelezaji wa mradi unavyoendelea, upanuzi wa majengo ya upasuaji, nyumba ya mganga, maabara, wodi ya mama na mtoto, nyumba ya kuhifadhia maiti, jengo la mionzi na kichomea taka.
Akikagua ukarabati huo Kandege ametoa maagizo yakiwamo ya Serikali izungumze na wananchi wanaoishi jirani na kituo cha Afya Matemanga ili kupisha upanuzi wa eneo la kituo cha Afya hadi kufikia ekari 8 kwa sasa ni ekari 4.
Pili, usimamizi uendelee kwa miradi ya afya inayoendelea hadi sasa Serikali imetoa Sh.milioni 500 katika kituo cha Afya Matemanga na Sh.milioni 400 katika kituo cha Afya Mkasale.Pia ameagiza wananchi wajitokeze kwa wingi kujiunga na huduma ya Afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa sasa waliojiunga Tunduru ni asilimia 43.5 ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.
Amefafanua huduma hiyi inapatikana kwa Sh.30,000 kwa mwaka na inajumuisha Mama Baba na watoto wa nne.Pia kujenga majengo ya mionzi kwa kila kituo cha afya ili kurahisha upatikanaji wa huduma ya Mama mjamzito na matatizo mengine yanayofanana na hayo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkasale Mkuu wa wilaya ya Tunduru Homera awewahakikishia wananchi Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli itaendelea kuleta fedha za maendeleo kwa wakati.
"Na kwa sasa fedha za ujenzi wa vitanda kwa ajili ya bweni la wasichana wa shule ya sekondari namasakata imetengwa zaidi ya Sh. milioni sita na umeme wa jua utafungwa hivi karibuni na sh. million 19 zitapelekwa shule ya sekondari Muhuwesi kujenga madarasa mawili inayotarajia kuanza kidato cha kwanza mapema 2019 Januari.Hapa kazi tu," amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akimkaribisha Naibu Waziri Ofis ya Rais Tamisemi,Mh. Josephati kandenge kazungumza na Wananchi wa kijiji cha Kasale kata ya Namasakata wilayani Tunduru,baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya Mkasale kinachojengwa na serikali ya awamu ya tano ya CCM kwa shilingini Millioni 400.
Naibu waziri Tamisemi Mh Josephat Kandege (wa tatu kulia) akiwa ameambatana Mkuu wa Wiaya ya Tunduru Mh.Juma Homera na viongozi wengine mbalimbali wakati wa ukaguzi wa kituo cha afya Mkasale ,Matemanga wilayani Tunduru na
Taarifa ya Ukaguzi wa nyumba ya mganga,maabara,mochwari,jengo la upasuaji la akina mama,wodi ya akina mama,kichoma taka, nk
Naibu Waziri Tamisemi Mhe Josephat kandege akitoa maelekezo kwa DC Homera
Hivyo makala NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFANYA ZIARA TUNDURU,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA TAIFA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFANYA ZIARA TUNDURU,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFANYA ZIARA TUNDURU,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA TAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/naibu-waziri-tamisemi-afanya-ziara.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFANYA ZIARA TUNDURU,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA TAIFA"
Post a Comment