Loading...
title : ZANTEL YAZINDUA PROGRAMU YA 'GRADUATE SALES FORCE PROJECT'
link : ZANTEL YAZINDUA PROGRAMU YA 'GRADUATE SALES FORCE PROJECT'
ZANTEL YAZINDUA PROGRAMU YA 'GRADUATE SALES FORCE PROJECT'
Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel imezindua programu yake ya 'Graduate Sales Force Project' yenye lengo la kuwapa ujuzi wahitimu wa vyuo vikuuambao bado hawajapata kazi rasmi kabla ya kuingia kwenye Soko la ajira.
Akizungumzia programu hiyo katika Makao makuu ya Kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Zantel, Haidari Chamshama alisema "Programu hii ni ya mwezi mmoja na ina lengo la kuwanufaisha wahitimu wa vyuo mbalimbali ambao bado hawana ajira rasmi kwa kufanya kazi kwenye vitengo mbalimbali katika Kampuni ya Zantel".
Kwa sasa programu hiyo itajikita kwenye Masuala ya Mauzo na wataangalia jinsi ambavyo wahitimu hao wanavyojituma kazini na hatimae kuajiri wachache kati yao.
Kwa Upande wake Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa alisema Soko la ajira limekua gumu kwa hivi sasa hivyo, Zantel wameona ni vyema kuwapa ujuzi wanahitimu wa vyuo mbalimbali ili kuwajengea ujuzi kabla ya kuingia ya kujipatia ajira.
Jumla ya wahitimu ni 95 kutoka vyuo 15 vya Tanzania wa fani tofauti wamechukuliwa kwa mwezi huu na Zantel kwa ajili ya mafunzo hayo kwa vitendo.
Meneja Mauzo na Usambazaji Zantel, Haidari Chamshama akizungumza na Wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini ambao wanafanyakazi kama Wauzaji wa huduma na bidhaa za Zantel leo katika makao Makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam kabla ya kutawanyika na kuelekea katika sehemu mbalimbali za kazi zao. Wahitimu hao wa vyuo vikuu wapo chini ya Programu ya Zantel iliyopewa jina la ‘Graduate Sales Force Project’ yenye lengo la kuwawezesha na kuwafundisha kwa vitendo ili kuwapatia ujuzi kabla ya kuingia kwenye Soko la ajira.
Hivyo makala ZANTEL YAZINDUA PROGRAMU YA 'GRADUATE SALES FORCE PROJECT'
yaani makala yote ZANTEL YAZINDUA PROGRAMU YA 'GRADUATE SALES FORCE PROJECT' Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZANTEL YAZINDUA PROGRAMU YA 'GRADUATE SALES FORCE PROJECT' mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/zantel-yazindua-programu-ya-graduate.html
0 Response to "ZANTEL YAZINDUA PROGRAMU YA 'GRADUATE SALES FORCE PROJECT'"
Post a Comment