Loading...

AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO

Loading...
AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO
link : AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO

soma pia


AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema kuwa anakerwa na wakandarasi wasio na uwezo, ambao wamekuwa wakitekeleza miradi bila kuzingatia mikataba, ama kutoikamilisha kwa wakati au kutekeleza chini ya kiwango kwa kukosa thamani halisi ya fedha iliyotumika.

Aweso alisema hayo wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya maji katika Wilaya ya Songea Vijjini, katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma na kusikitishwa na mwenendo wa utekelezaji usioridhisha wa baadhi ya miradi.

Naibu Waziri alisema kuwa ipo haja ya kufutiwa usajili na kutokupewa kazi yoyote nchini wakandarasi wote wababaishaji, baada ya kutoridhishwa tendaji wao katika baadhi ya miradi wilayani humo.

‘‘Hatutawavumilia wakandarasi wasio na uwezo ambao wanatuangusha, tutawafuatilia na ikiwezekana wafutiwe usajili kabisa nchini ili wasiendelee kufanya kazi mahali popote nchini, tubaki na wakandarasi wenye uwezo’’, alisema Aweso.

Akiwa mkoani Ruvuma, Aweso ametembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa katika wilaya za Tunduru, Namtumbo, Songea Mjini, Songea Vijijini na Madaba lengo likiwa ni kuweka msukumo katika utekelezaji wa miradi kwa nia ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati na wananchi wa mkoa huo wanapata huduma ya maji ya uhakika.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiangalia kilula cha maji cha mradi wa Liula, Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoa maagizo kwa watendaji mara baada ya kukagua Tenki la maji la mradi wa Parangu katika Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoka kukagua chanzo cha maji cha Masimeli, kinachotumika kuzalisha maji kwa ajili ya mradi wa Lipaya katika Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa kwenye tenki la mradi wa Matimila, Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.



Hivyo makala AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO

yaani makala yote AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/aweso-akerwa-na-wakandarasi-wasio-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AWESO AKERWA NA WAKANDARASI WASIO NA UWEZO"

Post a Comment

Loading...