Loading...
title : BENKI YA EXIM IPO MSTARI WA MBELE KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE HOSPITALI NCHI NZIMA.
link : BENKI YA EXIM IPO MSTARI WA MBELE KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE HOSPITALI NCHI NZIMA.
BENKI YA EXIM IPO MSTARI WA MBELE KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE HOSPITALI NCHI NZIMA.
Mkuu wa kitengo cha masoko cha Exim Bank Tanzania, Stanley Kafu pamoja na wafanyakazi wa tawi la Arusha wakikabidhi vitanda na magodoro 40 kwa mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dk Timothy Wonanji.
HOSPITALI na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Kama sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii, Benki ya Exim Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya mkoa ya Mount meru iliyoko Arusha.
Hospitali ya mkoa ya Mount Meru, Arusha, ni hospitali ya tano kupokea mchango huu, baada ya Hospitali ya rufaa Dodoma mwezi uliopita, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka huu. Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo na mgeni rasmi alikwa Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa, Arusha Dr Vivian Wonanji.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu alisema, “ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini. Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.”
Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa Arusha Dr. Vivian Wonanji alipongeza Exim Bank Tanzania kwa ahadi yake ya kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye ma hospitali ambao unakabiliwa na taifa na kuleta juhudi zake kwa hospitali ya mkoa ya Arusha. Afisa wa matibabu wa Hospitali ya mkoa, Mount Meru alisema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii.”
Ikiwa kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Mtwara, Pemba na Unguja ambapo mpaka sasa Dar es Salaam, Unguja, Mtwara, na Dodoma tayari wameshapokea misaada.
Hivyo makala BENKI YA EXIM IPO MSTARI WA MBELE KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE HOSPITALI NCHI NZIMA.
yaani makala yote BENKI YA EXIM IPO MSTARI WA MBELE KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE HOSPITALI NCHI NZIMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA EXIM IPO MSTARI WA MBELE KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE HOSPITALI NCHI NZIMA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/benki-ya-exim-ipo-mstari-wa-mbele.html
0 Response to "BENKI YA EXIM IPO MSTARI WA MBELE KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VITANDA KWENYE HOSPITALI NCHI NZIMA."
Post a Comment