Loading...
title : VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA
link : VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA
VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA
Said Mwishehe, Blogu ya jamii
MWENYEKITI wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(TID) Profesa Apollinaria Pereka amewataka vijana wasisite kuanzisha viwanda nchini kupitia elimu ya ufundi waliyoipata kwenye taasisi hiyo kwa manufaa ya taifa.
Pia amesema wasiogope changamoto watakazokumbana nazo na badala yake wawe wabunifu katika uanzishaji wa bidhaa zao.
Profesa Pereka amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye Mahafali ya 11 ya DIT ambapo amefafanua ,Serikali imejipanga kupiga vita umasikini, hivyo vijana ni vema wakaanzisha viwanda ili wajiajiri wenyewe.
Amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kulijenga taifa na kuanzisha viwanda endelevu.
Ameongeza nchi yenye maendeleo makubwa ni ile yenye ujuzi wa ufundi,na wanaotumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya uwanzishaji wa viwanda.
Pia amesema kwa sasa DIT imefikisha miaka 60 tangu ianzishwe na imefanya kazi kubwa kueneza elimu ya ufundi nchini.
“Utimizaji wa miaka 60 ya DIT imeenda sambasamba na serikali ya awamu ya tano ya kuanzisha viwanda nchini kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi ,hivyo tutakwenda sambamba na serikali hiyo ili kutimiza azma ya Rais, Dk. John Magufuli,"amesema
Awali Mkuu wa chuo hicho Profesa Preksedius Ndomba,amesema Serikali ya awamu ya tano inalenga kuleta maendeleo ya viwanda vidogo,vya kati na vikubwa.
"Hivyo vijana wajiunge katika vyuo vya ufundi ili kuweza kupata ajira na kuanzisha viwanda vyao wenyewe.
“Elimu ya ufundi ina umuhimu mkubwa katika serikali hii ya awamu yatano kwa sababu ya uwanzishaji wa viwanda nchini, vijana mjifundishe ufundi sanifu kwa ajili ya manufaa yenu wenyewe”amesisitiza Profesa Ndomba.
Ameongeza DIT ipo sambasamba na Serikali katika kufanikisha uanzishwaji wa viwanda, hivyo wapo makini katika utoaji wa elimu yao ili vijana wao wakimaliza wawe wasanifu wazuri katika viwanda vinavyokuja na kwamba wataendelea kupia watalaamu.
Mwenyekiti wa Baraza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT), Prof. Apollinaria Pereka akizungumza kwenye Mahafali ya 11 ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya wahitimu 876 wamehitimu ngazi mbalimbali za kitaaluma za Stashahda, Shahada na Shahada za Uhandisi na Teknolojia.
Hivyo makala VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA
yaani makala yote VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/vijana-wahamasishwa-kuanzisha-viwanda.html
0 Response to "VIJANA WAHAMASISHWA KUANZISHA VIWANDA"
Post a Comment