Loading...
title : BODI YA WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR WATEKETEZA DAWA ZA MENO
link : BODI YA WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR WATEKETEZA DAWA ZA MENO
BODI YA WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR WATEKETEZA DAWA ZA MENO
Na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Wafanyakazi kutoka Bodi ya Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar wameangamiza Tani tisa za Dawa ya meno aina ya Aloe zilizoharibika katika jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja
Dawa hizo ziliingizwa nchini na Kampuni ya Bacelona Interprises Limited zikiwa zimeharibika baada ya kontena lilikuwa na dawa hizo kuinga maji wakati wa kusafirishwa kuja Zanzibar .
Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Chakula Dawa Zanzibar Mwadini Ahmadi Mwadini alisema walibaini kuwa dawa hizo zimeharibika wakati wa kuzitoa bandarini na kumshauri mmiliki wa dawa hizo kuzirejesha zilikotoka au kuziangamiza na alikubali ziangamizwe ili kujiepusha na gharama nyengine.
Mwadini alisema Bodi inaendelea kufanya ukaguzi kwa bidhaa zinazoingizwa bandarini na maduka mbali mbali ili kuhakikisha zinakuwa salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Aliwataka wafanyabiashara kuwa waangalifu wanapoagiza Bidhaa na kujenga ushirikiano wa karibu na Bodi yake kwa kutowa taarifa wanapoona bidhaa zao zinamashaka kuuzwa kutokana na kuharibika au kupitwa na muda wake wa matumizi.Aidha aliwaomba wananchi wanaponunua bidhaa madukani na kuzigundua kuwa hitilafu watowe taarifa katika Bodi ili hatua zinazofaa ziweze kuchukuliwa kwa usala wao.
“Kama mukigundua kunafanyika udanganyifu kwa bidhaa mnazonunua kama kuharibika au kupitwa na wakati musisite kutoa taarifa kwetu, tupo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi.” alisema Mkaguzi Mkuu.
Wafanyakazi wa Bodi ya Wakala na Dawa Zanzibar wakiteremsha dawa za msuaki tani tisa zilizoharibika katika jaa la kibele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kuangamizwa.
Maboksi yaliyokuwa na dawa za msuaki zilizoharibika yakichomwa moto na wafanyakazi wa Bodi ya Wakala na Dawa Zanzibar katika jaa la Kibele, Wilaya ya Kati Unguja.
Gari aina ya kijiko likisaga dawa zilizoharibika ili kuziangamiza baada ya kuingia maji wakati wakusafirishwa katika jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.Picha na Ramadhani Ali – Maelezo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BODI YA WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR WATEKETEZA DAWA ZA MENO
yaani makala yote BODI YA WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR WATEKETEZA DAWA ZA MENO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BODI YA WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR WATEKETEZA DAWA ZA MENO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/bodi-ya-wakala-wa-chakula-na-dawa_17.html
0 Response to "BODI YA WAKALA WA CHAKULA NA DAWA ZANZIBAR WATEKETEZA DAWA ZA MENO"
Post a Comment