Loading...
title : Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China
link : Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China
Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China
Wziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Mambo ya Nje cha China kabla ya wawili hao hawajaelekea kwenye ukumbi kuhutubia wanafunzi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augastine Mahiga akihutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China. Dkt. Mahiga alieleza ushirikiano wa Tanzania na China ulipoanza hadi leo na kuwasihi wanafunzi hao waangalie namna y kuuimarisha kutokana na nafasi zao.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China wakisikiliza Hotuba ya Dkt. Mahiga. Wanafunzi hao ambao walikuwa wadadisi sana walifurahi sana kutokana na elimu ya siku moja waliopata kutoka kwa Mbobezi wa masuala ya Diplomasia.
Dkt. Mahiga akiendelea na hotuba yake huku Mkuu wa Chuo akisikiliza kwa makini. Mkuu huyo alikiri kuwa kutokana na hotuba hiyo amejifunza vitu vingi sana.
Ujumbe uliomsindikiza Waziri Mahiga, kutoka kulia ni Bw. Benedict Msuya, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Gerald Mbwafu, Katibu wa Waziri na Kanali Remigius Ng'umbi, Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.
Mstari wa Mbele kutoka kushoto ni Kamishna msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Malmeltha Mtagwaba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Thomas Kashililah, Naibu Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji kutoka Wizara ya Vwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wa Zanzibar, Bw. Khams Omar na Balozi wa Tnzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki wakifuatilia hotuba hiyo.
Hivyo makala Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China
yaani makala yote Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/dkt-mahiga-ahutubia-chuo-kikuu-cha.html
0 Response to "Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China"
Post a Comment