Loading...
title : KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA
link : KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA
KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA
Na WAMJW - Dodoma .
Madereva nchini wamepongezwa kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji unaofuata taratibu na sheria za barabarani.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania Fotunatus Mselemu –Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali .
Kamanda Mselemu alisema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike na kuboreka zaidi”Alisema.
Alisema hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto
Akitolea mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi nne,hivyo ni hatua nzuri.
Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu aliyesimama akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Mary Kessy akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
ASP Deus Sokoni wa kwanza kulia akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Mambo ya Ndani Bi. Marlin Komba anayefuata ni Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu.
Katibu Mkuu wa Shirikishi wa vyama vya Walemu nchini Bw. Felicina Mkude aliyesimama akiongea na baadhi ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA
yaani makala yote KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/kikao-cha-kujadili-hali-ya-usalama.html
0 Response to "KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA"
Post a Comment