Loading...

MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO

Loading...
MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO
link : MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO

soma pia


MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO

Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

MKOA wa Pwani ,tayari umeuza tani 19,815 ambazo zimeingiza zaidi ya bilioni 39 tofauti na msimu uliopita ambapo uliuza tani 13,000 na kupata bilioni 33.##

Mkoa huo umejiwekea lengo la kuuza tani 25,000 hadi 30,000 kwa msimu huu ambao minada yake ya korosho ikiwa bado inaendelea .Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliyasema hayo Mkuranga ,wakati akizungumzia changamoto na mafanikio waliyoyapata msimu wa korosho 2017/2018 .

Alieleza ,mbali ya hayo wakulima wa korosho mkoani Pwani wakiwa bado wanadai zaidi ya bilioni tano.Mhandisi Ndikilo alisema ,kuuza tani 19,815 hadi sasa ni mwanzo mzuri wa kufikia malengo yao waliyojiwekea msimu huu.Alisema ,hatua hiyo imetokana na serikali kutoa pembejeo bure katika msimu huu na mfumo wa stakabadhi ghalani.

Alibainisha ,licha ya mafanikio hayo lakini kuna changamoto zimejitokeza tangu kuanza kwa minada mwaka huu ikiwemo uhaba wa magunia .Kero nyingine ni ile iliyojitokeza sasa ya kuchakachua ubora wa korosho unaofanywa na baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika (Amcos).

“Changamoto ya magunia inaweza kuwa historia endapo tutakubaliana kwa kukaa na mikoa ya Lindi na Mtwara ili kuhamasisha wawekezaji waje wawekeze kiwanda cha magunia lengo likiwa ni kukabiliana na tatizo hili” alifafanua .Akizungumzia kuhusu tatizo la ubora wa korosho, mhandisi Ndikilo ,alisema baadhi ya Amcos zimejiingiza kwenye kuhujumu minada hiyo kwani baadhi yao wameweka michanga na mawe kwenye magunia ya korosho .
MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, ambae pia ni mkuu wa Mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo , akizungumza na baadhi ya wakulima wa korosho wakati alipotembelea ghala moja lililopo wilayani Mkuranga.Picha na Mwamvua Mwinyi




Hivyo makala MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO

yaani makala yote MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/mkoa-wa-pwani-umeuza-tani-19815-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MKOA WA PWANI UMEUZA TANI 19,815 ZA KOROSHO NA KUPATA BIL.39-RC NDIKILO"

Post a Comment

Loading...