Loading...

MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO

Loading...
MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO
link : MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO

soma pia


MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO


ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida,Marther Moses Mlata ameuagiza umoja wa vijana wa Chama hicho kutumia muda wanapokuwa kwenye makambi ya vijana kuwasaidia wazee  wanaosihi katika nyumba zinazotishia maisha yao kwa kuwajengea na kuwakabidhi wazee hao ili waweze kujihakikishia usalama wa maisha yao.
Mlata ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida alitoa agizo hilo wakati alipokuwa akimpokea mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida,Dk.Denisi Nyiraha alipokwenda kujitambulisha kwenye ofisi za chama hicho Mkoa wa Singida.
Aidha Mwenyekiti huyo aliyemaliza muda wake aliweka bayana kwamba kumekuwa kukifanyika makambi mengi sana na kambi hizo zimekuwa zikiwasaidia vijana kujifunza mambo mengi sana,lakini wakati vijana hao wanapokuwa makambini na kugundua kuna nyumba ya mkongwe mmoja inayokaribia kudondoka,watumie makambi hayo kuwasaidia wazee kama hao kunusuru maisha yao.
“Ukiwa kule unamuona ndani anavyozunguka,ninaomba makambi yale kama vijana tusaidieni wazee wale wasiangukiwe na nyumba zao na fanyeni taratibu yeyote mmeweka kambi mkifanya mafunzo yenu,lakini hakikisheni mnafyetua matofali na kuweka harambee kumjengea nyumba mpya na kumwambia bibi au babu ingia hapa”alisisitiza Mlata.  
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida,Dk.Denisi Nyiraha aliahidi kuunda kamati ndogondogo kuanzia ngazi ya wilaya hadi Mkoa ili kurahisisha majukumu ya mwenyekiti wa wilaya na Mkoa ikiwa ni pamoja na kuibua mipango mipya na endelevu ya kukuza na kujenga jumuiya.
Mwenyekiti huyo alisema ili kufanikisha azma hiyo ni wajibu wa kila wilaya ianze kujiandaa kuunda kamati ya sera na mipango kwenye ngazi ya Mkoa hadi katika ngazi za wilaya na kuitaja kamati nyingine atakayounda ni kamati ya uchumi itakayokuwa na wajibu wa kwenda kubaini vyanzo vya jumuiya katika ngazi hizo.
“Kwa hiyo kamati hii itakuwa na wigo mpana na kwa mfano nitolee majukumu ya kamati hii ya uchumi ngazi ya mkoa,tutaunda chombo kitakachokwenda kufanya auditing,kitakachoenda kufanya upembuzi yakinifu kwenye miradi yote kwenye ngazi ya Mkoa”alisisitiza Dk.Nyiraha.
Hata hivyo Dk.Nyiraha alitumia fursa ya kikao hicho kutoa angalizo kwa kiongozi yeyote yule iwapo alishiriki kwa njia yeyote ile katika matumizi mabovu ya miradi na iwapo kuna fedha ambazo bado anazo aliagiza azirudishe bado mapema.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wale wote waliohusika kuhujumu mali za chama,mali za umoja wa vijana wajiandae kuzirejesha maana hawatafumbiwa macho na kwamba miradi yote ya chama kuanzia ngazi ya wilaya ambayo imetaifishwa na vyombo tofauti tofauti waliombwa kuvirejesha haraka iwezekanavyo,
Hata hivyo katika risala wa chipukizi iliyosomwa kwa Mwenyekiti huyo wa UVCCM,imeeleza changamoto zinazowakabili vijana hao kuwa ni pamoja na kutokuwa na sare za kijani na suruwali nyeusi na wanatarajia kuwa ombi lao watatekelezewa.


Hivyo makala MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO

yaani makala yote MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/mlata-aagiza-makambi-ya-uvccm.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MLATA AAGIZA MAKAMBI YA UVCCM KUWAJENGEA NYUMBA VIKONGWE WANAOISHI KWENYE NYUMBA ZINAZOTISHIA MAISHA YAO"

Post a Comment

Loading...