Loading...
title : WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018
link : WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018
WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ameutaka uongozi wa Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) kuangalia na kupitia nyaraka walizonazo ili kuona uhalali wa umiliki wa eneo la hekta 20000 kwenye vitalu tisa vilivyomo kwenye Ranchi ya Uvinza inayomilikiwa na Kampuni ya Ranchi za za Mifugo za Taifa (NARCO)kabla ya Selikali kuwatoa kwa nguvu ifikapo tarehe 1/1/2018.
Waziri Mpina ametoa maelekezo hayo leo alipotembelea Ranchi ya Uvinza kuangalia shughuli mbalimbali katika Ranchi hiyo ambapo ametoa muda wa hadi Januari mosi mwakani kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo endapo atabaini kuwa amekuwa akikaa kimakosa kuanzia katika vitalu namba 41 hadi 49.
Aidha Waziri Mpina amesema endapo Mwekezaji huyo ataendelea kubaki baada ya tarehe Mosi Januari, Serikali itamuondoa kwa nguvu na atatakiwa kulipa gharama zote za fidia na usumbufu.“Ninakuagiza angalia taarifa mbalimbali ulizonazo kuhusu umiliki wa eneo hili kama utaona umeendelea kukaa hapa bila kufuata taratibu tafadhali uondoke mara mmoja ili kupisha Serikali kuendelea na shughuli zake” alisisitiza Mpina
Waziri Mpina amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa Philemoni Wambura kuwaandikia barua ya kuwaondoa wawekezaji wote katika Ranchi hiyo ambao hawajaendeleza kwa zaidi ya asilimia 40 na kwamba wawekezaji ambao wamewekeza kwa zaidi ya asilimia arobaini wanatakiwa kukamilisha malipo yote kabla ya Januari mosi mwakani.
Alionya wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kwamba wanauwezo wa kuwekeza katika vitalu ili wapewe lakini wanabadili matumizi baada ya kupewa. Aliongeza kwamba Serikali imegundua baadhi ya wawekezaji wanaopewa vitalu wanawakodisha wafugaji kutoka nchi jirani na kujipatia faida wakati Serikali haipati chochote.
Awali, Meneja wa (TGTS) Audax Kalulama akizungumza kwa simu na Waziri Mpina kutoka Arusha amesema kwamba eneo hilo wanamiliki kihalali na kuomba muda ili wawasiliane na Wizara ya Mifugo kuonyesha taarifa za umiliki wa eneo hilo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina akizungumuza na Meneja wa Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) Audax Kalulama katika simu alipotembelea Ranchi ya Uvinza leo na kuamuru mwekezaji huyo kuondoka kabla ya Januari Mosi mwakani kutokana na Mwekezaji huyo kukaa katika eneo hilo kinyume cha Sheria.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina (katikati) kitoa maamuzi ya kuitaka Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) kuondoka katika eneo la hekta 20000 kwenye vitalu tisa vilivyomo kwenye Ranchi ya Uvinza ifikapo tarehe 1/1/2018.
Sehemu ya Ranchi ya Uvinza.
.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina (katikati) akiwasikiliza walinzi wa Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) hawapo pichani wakitoa maelezo alipotembelea Ranchi ya Uvinza .
Hivyo makala WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018
yaani makala yote WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/waziri-mpina-aitaka-kampuni-ya-game.html
0 Response to "WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018"
Post a Comment