Loading...
title : RC MBEYA AMOS MAKALA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYORATIBIWA NA WCF
link : RC MBEYA AMOS MAKALA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYORATIBIWA NA WCF
RC MBEYA AMOS MAKALA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYORATIBIWA NA WCF
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mbeya
TAKRIBAN madaktari na watoa huduma za afya 100 kutoka mikoa saba ya Kanada ya Nyanda za Juu Kusini, wameanza kupatiwa mafunzo jijini Mbeya yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF).
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo ya siku tano yaliyofunguliwa rasmi Desemba 12, 2017 (jana) NA Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba, alisema, mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo kwa madaktari na watoa huduma za afya ili kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini ya ulemavu maradhi anayopata mfanyakazi wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi ili hatimaye madaktari hao waweze kutoa mapendekezo kuwezesha mfuko kutoa mafao ya fidia stahiki.
Kwa mujibu wa mratibu wa mafunzo hayo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, mafunzo hayo yamewaleta pamoja madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe, Katavi, Rukwa, Iringa, Njombe na Ruvuma.
Katika hatua ya kuimarisha Hifadhi ya Jamii, Tanzania, Serikali ilianzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, kipengele cha 263 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2015 ili kuhakikisha kila mfanyakazi Tanzania Bara kutoka sekta ya umma na binafsi anapata fursa ya kuwekewa bima na mwajiri wake ili anapopata majeraha au magonjwa awapo kazini basi aweze kufidiwa kwa mujibu wa sheria, alisema Bw. Mshomba.
“Lengo kuu la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kutoa fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyepatwa na majeraha, maradhi kutokana na kutekeleza wajibu wake awapo kazini, lakini pia kuwalipa fidia wategemezi wake anapofariki katika mazingira hayo.” Alifafanua Bw. Mshomba na kuongeza, WCF ilianza kutekeleza majukumu yake Julai Mosi, 2015 na mwaka uliofuata Mfuko ulianza rasmi kupokea madai ya fidia na kulipa mafao kwa waathirika.
Wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa WCF jijini Arusha mwishoni mwa mwezi uliopita, kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, aliitaka WCF kuendelea kutoa elimu kwa wadau, ili waweze kuelewa vema shughuli za Mfuko na nia njema ya serikali ya kuanzisha mfuko huo ili mfanyakazi wa Tanzania aweze kupata fidia stahiki anapopata madhara sehemu ya kazi.
Bw, Mshomba aliishukuru Serikali na Wizara zake kwa kuunga mkono na kusaidia juhudi za WCF katika kuimarisha mifumo yake ili kutoa huduma bora kwa wadau wake.“Pia napenda nizishukuru taasisi za Hospitali ya Taifa Muhimbili, MOI, Ocea Road Hospital, MUHAS, na OSHA kwa kuwaruhusu wataalamu wake ili tuwatumie katika kutoa mafunzo haya.” Alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Amos Makala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo, alisema, juhudi za ushirikiano wa pamoja miongoni mwa wadau yaani Serikali, Wafanyakazi, Waajiri unahitajika sana kuhakikisha tathmini endelevu ili kuimarisha mfuko.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala, akihutubia wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo Desemba 12, 2017. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu au ugonjwa mahali pa kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfukom wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba ya ukaribisho kweye ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo Desemba 12, 2017. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na WCF, yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu au ugonjwa mahali pa kazi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala, na Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Hivyo makala RC MBEYA AMOS MAKALA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYORATIBIWA NA WCF
yaani makala yote RC MBEYA AMOS MAKALA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYORATIBIWA NA WCF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MBEYA AMOS MAKALA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYORATIBIWA NA WCF mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/rc-mbeya-amos-makala-afungua-mafunzo-ya.html
0 Response to "RC MBEYA AMOS MAKALA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYORATIBIWA NA WCF"
Post a Comment