Loading...
title : Siri ya Zanzibar Heroes kufanya vizuri yatajwa: Ni Umoja wetu
link : Siri ya Zanzibar Heroes kufanya vizuri yatajwa: Ni Umoja wetu
Siri ya Zanzibar Heroes kufanya vizuri yatajwa: Ni Umoja wetu
Kiungo wa Zanzibar Heroes, Abdul Aziz Makame ambae aliifungia Zanzibar Heroes goli la kwanza dhidi ya Uganda Cranes na kuchaguliwa nyota wa mchezo Man of the match.
Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.
Kiungo wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Abdul aziz Makame (Abui) ameweka hadharani siri kubwa iliyowapelekea kufanya vyema katika Mashindano ya Cecafa Senior Challenge Cup yanayoendelea nchini Kenya.
Makame amesema umoja wao ndio silaha kubwa kwao mpaka wakafanikiwa kutinga fainali katika Mashindano hayo.
“Sisi tunapendana sana, yani tuna umoja wa hali ya juu sote wachezaji, viongozi mpaka Mashabiki wetu, tunapokosea tunafahamishana kwa lengo la kutengeneza si kubomoa ndio maana sasa tumefika fainali”. Alisema Makame.
Makame alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo (Man of the Match) katika mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Zanzibar na Uganda ambapo Zanzibar ilishinda 2-1 na kesho Jumapili saa 9:00 Alaasiri Zanzibar itacheza fainali na wenyeji Kenya mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya.
Hivyo makala Siri ya Zanzibar Heroes kufanya vizuri yatajwa: Ni Umoja wetu
yaani makala yote Siri ya Zanzibar Heroes kufanya vizuri yatajwa: Ni Umoja wetu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Siri ya Zanzibar Heroes kufanya vizuri yatajwa: Ni Umoja wetu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/siri-ya-zanzibar-heroes-kufanya-vizuri.html
0 Response to "Siri ya Zanzibar Heroes kufanya vizuri yatajwa: Ni Umoja wetu"
Post a Comment