Loading...

ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA

Loading...
ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA
link : ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA

soma pia


ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA

Na Mwandishi Wetu
MKOA wa Dar es Salaam umeipatia Ngao Maalum shule ya St. Anne Maria kama sehemu ya kutambua mchango wake katika kuinua elimu hapa nchini.

Sherehe ya kuzawadia shule zilizofanya vizuri ilifanyika mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Thelesia Mbando, kwenye kilele cha siku ya elimu Dar es Salaam, zilizofanyika ukumbi wa PTA Sabasaba.

Shule hiyo ilipewa ngao inayoonyesha kuwa ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2016, Best Performing Primary School in Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kupokea ngao hiyo, Mkuu wa Shule hiyo, Gladius Ndyetabura alisema ngao hiyo imewapa changamoto ya kuendelea kufundisha kwa bidii ili hatimaye wapate matokeo mazuri zaidi ya mwaka huu.

Alisema ingawa shule yake imefanikiwa kuingia kumi bora kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, lakini hawajabweteka na badala yake wanafanya jitihada za kuwa namba moja.

“Kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu tumefanikiwa kuwa wa kwanza Wilaya ya Ubungo, tumekuwa wa pili Mkoa wa Dar es Salaam na tumekuwa wanane kitaifa sasa hii haitufanyi tubweteke tutapambana kupata nafasi za juu zaidi,” alisema  

Aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwapa ngao hiyo ambayo imewapa motisha na ari ya kuendelea kufundisha kwa bidiii ili kupata matokeo mazuri zaidi ya waliyopata mwaka huu.

“Shule ni nyingi na ushindani ni mkubwa sana hivyo bado tunakazi ya kufanya kuhakikisha tunaendelea kuwa kumi bora na hata kuwa wa kwanza kitaifa, ingawa shule ni nyingi sana hapa Dar es Salaam lakini tuliopewa ngao na vyeti ni wachache sana sasa hii inaonyesha namna gani mchango wetu unavyothaminiwa,” alisema
Mwalimu Mkuu wa Shule ya St Anne Maria ya Mbezi kwa Msuguri, Gladius Ndyetabura akifurahia pamoja na wanafunzi wa shule hiyo ngao ambayo shule hiyo imepewa na Mkoa wa Dar es Salaam kuipongeza kwa kufanikiwa kuwa ya nane kitaifa na ya kwanza Wilaya ya Ubungo kwenye matokeo ya darasa la saba.


Hivyo makala ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA

yaani makala yote ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/st-anne-maria-yapewa-ngao-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ST ANNE MARIA YAPEWA NGAO KWA KUFAULISHA LASABA"

Post a Comment

Loading...