Loading...
title : AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA
link : AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA
AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA
Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limeendesha warsha kwa WAVIU Washauri 75 kutoka halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).
WAVIU washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa,kutoa ushauri nasaha kwa wenzao,kujitolea kufuatilia na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha WAVIU wenzao kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.
Warsha hiyo ya siku tatu imeanza Jumatatu Januari 29,2018 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja WAVIU Washauri takribani 75 kutoka halmashauri za wilaya za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga, Kahama Mji, Ushetu na Msalala.
Akizungumza katika warsha hiyo, Mratibu wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo WAVIU Washauri ili waweze kuwaunganisha wateja kutoka kwenye jamii kwenda kwenye vituo vya tiba na matunzo na kuwafuatilia wateja waliopotea katika huduma na kuwarudisha kwenye huduma.
“Kupitia warsha hii tutapeana mikakati mbalimbali jinsi ya kuwatafuta wateja waliopotea katika huduma na kujadili namna ya kuboresha zaidi huduma katika vituo vya tiba na matunzo lakini pia kutoa elimu kuhusu haki za WAVIU Washauri”,alieleza Tesha.
Mratibu wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya WAVIU Washauri halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga.
Aminael Tesha akielezea malengo ya warsha hiyo.
Mwezeshaji katika warsha hiyo,Vedastus Mutangira akitoa elimu kuhusu VVU na Ukimwi. Aliwasisitiza watu wanaoishi na VVU kumeza dawa kwa utaratibu sahihi uliowekwa pamoja na kuhudhuria kliniki mara kwa mara.
MVIU Mshauri Neema Anthony kutoka kutoka CTC ya Segese katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA
yaani makala yote AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/agpahi-yaendesha-warsha-kwa-waviu.html
0 Response to "AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA"
Post a Comment