Loading...
title : ISRAEL KUJENGA KITENGO CHA DHARULA NA TIBA YA MIFUPA MKOANI DODOMA
link : ISRAEL KUJENGA KITENGO CHA DHARULA NA TIBA YA MIFUPA MKOANI DODOMA
ISRAEL KUJENGA KITENGO CHA DHARULA NA TIBA YA MIFUPA MKOANI DODOMA
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI ya Tanzania imesaini makubaliano na Serikali ya Israel ya ujenzi wa kitengo cha dharula na tiba ya mifupo katika hospitali ya Benjamini mkoani Dodoma.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk.Otilia Gowelle amesema kuwa ujenzi wa kitengo hicho utasaidia katika utoaji wa huduma za afya zilizo bora.
Amesema kitengo hicho kitajengwa na Serikali ya Israel ikiwa ni pamoja na madaktari nchini kujengewa uwezo katika utoaji wa huduma katika kitengo hicho.Dk. Gowelle amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Israel na Tanzania ni uhusiano imara katika kusaidia utoaji huduma katika sekta ya afya.
.Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Otilia Gowelle akisaini makubaliano na Naibu Balozi wa Israel Nchini, Michael Baror ya ujenzi wa kitengo cha dharula na tiba ya mifupa katika Hospitali ya Benjamini mkoani Dodoma, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Otilia Gowelle akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Balozi wa Israel Nchini, ,Michael Baror ya ujenzi wa kitengo cha dharula na tiba ya mifupa katika Hospitali ya Benjamini mkoani Dodoma, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Otilia Gowelle na Naibu Balozi wa Israel Nchini,Michael Baror pamoja na watendaji mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini makubaliano ya ujenzi wa kitengo cha dharula na tiba ya mifupa katika Hospitali ya Benjamini mkoani Dodoma, leo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala ISRAEL KUJENGA KITENGO CHA DHARULA NA TIBA YA MIFUPA MKOANI DODOMA
yaani makala yote ISRAEL KUJENGA KITENGO CHA DHARULA NA TIBA YA MIFUPA MKOANI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ISRAEL KUJENGA KITENGO CHA DHARULA NA TIBA YA MIFUPA MKOANI DODOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/israel-kujenga-kitengo-cha-dharula-na.html
0 Response to "ISRAEL KUJENGA KITENGO CHA DHARULA NA TIBA YA MIFUPA MKOANI DODOMA"
Post a Comment