Loading...
title : MRADI WA MAJI NA JENGO LA UZAZI ZAHANATI YA YOMBO/BAGAMOYO YAKWAMA
link : MRADI WA MAJI NA JENGO LA UZAZI ZAHANATI YA YOMBO/BAGAMOYO YAKWAMA
MRADI WA MAJI NA JENGO LA UZAZI ZAHANATI YA YOMBO/BAGAMOYO YAKWAMA
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo.
Wakazi wa kijiji cha Yombo kata ya Yombo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamelalamikia mradi wa maji uliofadhiliwa na Bank ya Dunia na kugharimu milioni 297, ambao haufanyikazi huku wakiwa hawanufaiki nao tangu ukamilike.
Aidha wamelalamikia kukwama kwa mradi wa jengo la uzazi, katika zahanati ya Yombo,ambalo limetumia kiasi cha sh.mil.55 na kuwekwa jiwe la msingi na katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa,Abdulrahman Kinana tangu mwaka 2014.
Kilio hicho kimetolewa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho ,wakati wa mkutano wa wananchi uliomwita diwani wa kata ya Yombo ,Mohammed Usinga kwenda kuwaeleza hatua zinazochukuliwa ili kukamilisha miradi hiyo .
Mkazi wa Yombo,Jabir Omary ,alisema inasikitisha kuona serikali na wafadhili wanatumia mamilioni ya fedha kwenye miradi ya maendeleo lakini haiendelezwi na haifanyikazi.
Alieleza mradi huo wa maji umetumia fedha nyingi ,hivyo ni jukumu la serikali kuisimamia ili ilete tija ndani ya jamii.Mkazi mwingine ,Abubakar Harubu alimtaka diwani wa kata hiyo pamoja na bodi ya maji ya kata kufuatilia na kusimamia kero hizo kwa maslahi ya wakazi hao.
Diwani wa kata ya Yombo wilayani Bagamoyo, Mohammed Usinga akizungumza na wakazi wa kijiji cha Yombo kuhusiana na baadhi ya miradi ya maendeleo isiyofanyakazi na mengine kushindwa kuendelezwa.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Jengo la wodi ya uzazi katika zahanati ya Yombo, Bagamoyo likiwa limekwama kwenye ujenzi na kuwekwa jiwe la msingi na katibu mkuu wa CCM Taifa ,Abdurahman Kinana mwaka 2014 .
Mradi wa maji uliofadhiliwa na bank ya dunia na kugharimu mamilioni ya fedha huko kata ya Yombo Bagamoyo, ambao haufanyi kazi iliyotarajiwa na wananchi hawanufaiki nao tangu ukamilike 2015.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MRADI WA MAJI NA JENGO LA UZAZI ZAHANATI YA YOMBO/BAGAMOYO YAKWAMA
yaani makala yote MRADI WA MAJI NA JENGO LA UZAZI ZAHANATI YA YOMBO/BAGAMOYO YAKWAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MRADI WA MAJI NA JENGO LA UZAZI ZAHANATI YA YOMBO/BAGAMOYO YAKWAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/mradi-wa-maji-na-jengo-la-uzazi.html
0 Response to "MRADI WA MAJI NA JENGO LA UZAZI ZAHANATI YA YOMBO/BAGAMOYO YAKWAMA"
Post a Comment