Loading...

MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji

Loading...
MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji
link : MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji

soma pia


MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji

Kuanza safari kwa Meli za kisasa za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma ambazo zina uwezo wa kubeba uzito wa tani 1,000 kumefungua fursa za kibiashara kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji.

Meli ya Mv Njombe ambayo imefanya safari yake kwa mara ya kwanza nchini Malawi imefika salama na kutia nanga katika bandari za Nkhata Bay. Meli ya Mv Ruvuma inayopakia shehena ya Clinker inatarajiwa kutia nanga katika Bandari ya Monkey Bay nchini Malawi siku mbili zijazo.MV Njombe ambayo ilibeba takribani tani 800 ya shehena ya saruji kutoka bandari ya Kiwira nchini Tanzania hadi bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi imetia nanga salama na imetumia muda mfupi zaidi kufika Malawi.

MV Ruvuma ambayo ni pacha wa MV Njombe nayo imepakia takribani tani 800 za shehena ya ‘Clinker’ katika bandari ya Kiwira nchini Tanzania kuelekea bandari ya Monkey bay nchini Malawi.Akizungumzia ujio wa shehena hizo za Saruji na ‘Clinker’, Balozi wa Tanzania nchini Malawi ambaye pia alikuja kushuhudia tukio hilo, Mheshimiwa Benedicto Mashiba amesema kwamba kuanza kwa safari hizo ni habari njema kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Malawi .

Balozi Mashiba amesema kwamba, ujio wa meli hizo ni ufunguo wa biashara kati ya Tanzania na Malawi kwani kusafirisha bidhaa kwa njia ya maji ni nafuu na salama zaidi ukilinganisha na barabara.

“Usafiri huu ni mkombozi kwa wananchi na wafanyabiashara wa nchi hizi mbili (Malawi na Tanzania) kwani utawezesha usafirishaji wa mizigo kwa wingi ukilinganisha na njia nyingine kama barabara,” amesema Balozi Mashiba.Mashiba amesema kwamba kuna biashara kubwa ya kusafirisha mizigo kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji kupitia Ziwa Nyasa hivyo kuanza safari kwa meli hizo kutasaidia kuongeza zaidi ukubwa wa shehena katika ya nchi hizo.
 Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kushoto, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex Mdooa mara baada ya meli kuwasili bandarini hapo
 Mkuu wa bandari za Ziwa Nyasa, Ajuaye Msese kushoto, akitoa maelezo kwa Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kulia, katikati kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex Mdooa
 MV Njombe ilipowasili bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi
MV Njombe mara baada ya kutia nanga bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji

yaani makala yote MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/mv-njombe-yafungua-fursa-za-biashara.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MV Njombe yafungua fursa za biashara Tanzania, Malawi na Msumbiji"

Post a Comment

Loading...