Loading...

Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata

Loading...
Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata
link : Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata

soma pia


Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata

Mwambawahabari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Januari, 2018 amewajulia hali baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam wakiwemo Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti.

Katika wodi ya Mwaisela, Mhe. Rais Magufuli amemjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambaye anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa wake, nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Ibrahim Mkoma wa hospitali hiyo amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa hali ya Mzee Kingunge inaendelea vizuri.

Mzee Kingunge amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kwenda kumuona hospitalini hapo na amemueleza kuwa sasa anajisikia nafuu baada ya kupata matibabu.

Pamoja na kumpa pole na kumuombea apone haraka Mhe. Rais Magufuli amesema anatambua mchango mkubwa wa Mzee Kingunge katika siasa na maendeleo ya nchi.

Katika wodi ya Sewahaji, Mhe. Rais Magufuli amemjulia hali Bw. Richard Kajumulo ambaye ni Kaka wa Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Bw. Said Abeid Salim, Bi. Amina Ismail Shirwa, Mzee Hamad Lila na amempa pole Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula aliyefiwa na Mama yake mzazi wakati Mhe. Rais akiwa wodini humo.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amewajulia hali mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa matibabu ya moyo.

Maria na Consolata wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kwenda kuwaona na kuwapa pole na pia wameongoza sala ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli na nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi amesema matibabu kwa Maria na Consolata ambao ni wanafunzi mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Ruaha (RUCU) yanakwenda vizuri.

Aidha, Prof. Janabi amesema taasisi hiyo imefanikiwa kutoa matibabu kwa wagonjwa wa moyo 1,400 katika mwaka uliopita na kwamba inashika nafasi ya tatu barani Afrika kwa utoaji wa huduma bora za matibabu ya moyo.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza madaktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa wanayofanya kutibu wagonjwa na amesema Serikali itaendelea kutatua changamoto zinazowakabili ili kuboresha huduma zaidi.

“Nawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote, mnafanya kazi kubwa ya kuwatibu wagonjwa, pia mmeboresha hospitali na inaonekana ni safi, mimi niwaahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira yenu ya kazi ili muendelee kutoa huduma nzuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.



Hivyo makala Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata

yaani makala yote Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/rais-magufuli-awatembelea-hospitalini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Rais Magufuli awatembelea hospitalini mapacha walioungana, Maria na Consolata"

Post a Comment

Loading...