Loading...
title : UFUNGUZI WA BANDARI YA MKOKOTONI ZANZIBAR
link : UFUNGUZI WA BANDARI YA MKOKOTONI ZANZIBAR
UFUNGUZI WA BANDARI YA MKOKOTONI ZANZIBAR
Na Khadija Khamis –Maelezo 03/01/2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed amewataka wafanyakazi wa shirika Bandari Zanzibar kufanya kazi kwa bidii na kujenga uadilifu ili kuipatia pato serikali pamoja na kuleta maendeleo katika nchi.
Kauli hiyo ameieleza leo huko katika ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Shirika la Bandari Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya sherehe ya miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Alisema wafanyakazi waweze kupambana katika kuhakikisha wanazuia rushwa na uingizaji wa biashara haramu jambo ambalo linaharibu nguvu kazi ya taifa na kuipunguzia pato serikali
“Lazima wafanyakazi wadhibiti kuvuja mapato kama hakuna mapato katika serikali na maendeleo hayapo na kipato hakiwi ikiwa kinatumiwa kwa ubadhirifu ” alisema Waziri .
Aidha alisema juhudi za serikali ni kutekeleza ilani ya chama ambayo inalengo la kuwaletea maendeleo mbali mbali wananchi wake bila ya upendeleo na kusimamia utekelezaji wa ahadi jambo ambalo ndio malengo makuu ya Mapinduzi .
Alifahamisha serikali inatoa huduma kwa wananchi wote bila ya kuwa na ubaguzi wa rangi wala jinsia yoyote katika sekta mbali mbali za serikali pamoja na njanja tofauti za kisiasa kiuchumi na kijamii .
Alisema bandari ndogo ndogo zina mtindo wa kupitisha biashara ya haramu ikiwemo madawa ya kulevya na kutumia mbinu mbali mbali za kuichafua nchi hivyo alizitaka taasisi husika kuchukua juhudi za kukabiliana nazo.
Alieleza kuwa Zaidi ya Shilling Million 378 zilizotumika katika Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Shirika la Bandari la Mkokotoni na kuhakikisha kuwa si muda mrefu utaanza ujenzi wa gati ambalo linatarajiwa liwe la kisasa lenye hadhi inayolingana na mkoa huo.
Nae katibu Mkuu wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe amesema ujenzi huu ni utekelezaji wa ilani ya chama ambayo aliahidi Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ni moja ya ahadi zake za kuhakikisha anaimarisha maendeleo ya miundo mbinu ya Mkoa Kaskazini kwa kutekeleza ahadi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya Bandari pamoja na Gati mpya ya mkokotoni ambayo inatarajia kuchukua mizigo ya uzito wa tani mia moja.
Aidha alisema ujenzi wa bandari hiyo inakusudiwa kutumia Zaidi ya Tsh,Bilioni moja na Million 800 na gati hiyo inatarajiwa kuwa na urefu wa mita 170 na upana wa mita sita bandari hiyo inasafirisha abiria kwa kwenda na kurudi pamoja na mizigo mkaa mbao pamoja na dhamani .
Shirika la Bandari lilianzishwa mwaka 1997 ikiwa ni muunganiko wa Idara mbili ikiwemo Idara ya Bandari pamoja na Zanzibar Ofeji kwa lengo la kuleta ufanisi na kuimarisha uchumi wa Zanzibar.
Hivyo makala UFUNGUZI WA BANDARI YA MKOKOTONI ZANZIBAR
yaani makala yote UFUNGUZI WA BANDARI YA MKOKOTONI ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UFUNGUZI WA BANDARI YA MKOKOTONI ZANZIBAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/ufunguzi-wa-bandari-ya-mkokotoni.html
0 Response to "UFUNGUZI WA BANDARI YA MKOKOTONI ZANZIBAR"
Post a Comment