Loading...

Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...!

Loading...
Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...! - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...!, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...!
link : Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...!

soma pia


Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...!

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa jana usiku amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini mawakala wa meli wanaotoa huduma katika bandari hiyo hawafanyi kazi saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.

Prof. Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa mawakala wote waliokiuka agizo la Serikali la kutoa huduma bandarini kwa saa 24.

"Kati ya Mawakala wa Meli nane ambao tumewatembelea usiku huu ni wakala mmoja tu ndiye tuliyemkuta akitoa huduma kwa saa 24 hivyo SUMATRA katika kipindi cha siku saba hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe kwa wote wanaokiuka utaratibu huu na nipewe ripoti ya hatua zilizochukuliwa," alisema Waziri Prof. Mbarawa.

"Katika ukaguzi huu tumegunduwa kuwa mawakala wengi wanaacha watoa huduma wasiostahili, wakiwemo walinzi kufanya kazi nyakati za usiku ambao hawawezi kutoa huduma inayostahili usiku na kuendelea kutoa huduma asubuhi jambo ambalo sio sahihi," amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwa simu na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisini kwake.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), wakishuhudia moja ya wakala wa meli akiwa amefunga ofisi kinyume cha maelekezo ya Serikali ya kufanya kazi saa 24.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...!

yaani makala yote Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...! Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...! mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/waziri-profesa-mbarawa-avamia-bandarini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Waziri Profesa Mbarawa avamia bandarini Usiku, abaini madudu...!"

Post a Comment

Loading...