Loading...
title : MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI
link : MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI
MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI
Na Wankyo Gati, Arusha
UHABA wa fedha na watumishi katika uendeshaji wa shughuli za Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ), unachangia kukwamisha baadhi ya mashauri mahakamani hapo.
Akielezea changamoto zinazoikabili mahakama hiyo jana mjini hapa ofisini kwake Rais wa EACJ Jaji Dk. Emmanuel Ugerashebuja alizitaja changamoto mbili kubwa kuwa ni fedha pamoja na watumishi.
“Mambo haya ni kizungumkuti kinachotukabili hapa, upatikanaji kwa wakati fedha za kutusaidia kuendesha shughuli za mahakama kwa wakati imekuwa changamoto,” alisema Dk. Ugerashebuja na kuongeza:
“Jambo hili linatufanya kushindwa kufikia malengo kama EACJ tuliyopangiwa kwenye mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya yenyewe lakini pia Mahakama hii,” alisema
Dk. Ugerashebuja aliendelea kufafanua changamoto nyngine kuwa ni uhaba wa wafanyakazi wanaowasaidia Majaji mahakamani hapo kutekeleza shughuli za kila siku za Kimahakama.
“Kwa kweli tunaona jinsi ambavyo nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliosaida kuanzisha mahakama hii wanavyojaribu kutafuta dawa ya changamoto hizi zinazototkabili,” alisema Dk. Ugerashebuja.
Alisema uhitaji huo wa wafanyakazi kwa sasa umekuwa mkubwa kutokana na mahakama hiyo kuwa na kesi 282 ikilinganishwa na kesi moja iliyofunguliwa mwaka 2001 walipokuwa wakiapishwa majaji wa kwanza.
“Kwa sasa tuna kesi nyingi sana ukiangalia histroria yetu nyuma tuliwahi kuwa na kesi moja baada ya miaka minne tangu kuanzishwa,” alisema Dk. Ugerashebuja.
Aidha Rais huyo wa EACJ aliyataja mafanikio waliyoyapata tangu kuanzishwa kwa mahakama hiyo kuwa ni pamoja na kufunguliwa kwa ofisi za Msajili katika kila nchi mwanachama.
Kwa upande wake Msajili wa Mahakama Yufnalis Okubo alisema kwa sasa mahakama hiyo ina wafanyakazi 28 huku uhitaji ukiwa ni wafanyakazi 10 wenye taaluma mbalimbali.
“Kwa sasa mahakama hii imeendelea kupokea kesi nyingi tukifanikiwa kuongeza wafanyakazi 10 tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuendelea kutekeleza yale tuliyopangiwa.
“Hapa kuna kesi nyingine zimefunguliwa zihusisha Taasisi mbili za Serikali zilizoshitakiana na wamekuja kwenye mahakama hii,” alisema Msajili Okubo na kuongeza:
“Hawakuchangua kwenda kwenye mahakama zilizopo kwenye nchi zao wamekuja hapa, kwanini wanaamini watapata uamuzi sahihi kwenye mashauri waliyoshitakiana,” alisema.
Mwisho.
Kushoto ni Rais wa eacj jaji dr Emmanuel Ugerashebuja na kulia ni Msajili wa Mahakama hiyo Yufnalis Okubo
Hivyo makala MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI
yaani makala yote MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mahakama-ya-jumuiya-ya-afrika-mashariki.html
0 Response to "MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI"
Post a Comment