Loading...
title : MOHAMMED DEWJI APONGEZA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KUFUFUA VIWANDA
link : MOHAMMED DEWJI APONGEZA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KUFUFUA VIWANDA
MOHAMMED DEWJI APONGEZA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KUFUFUA VIWANDA
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji akizungumza katika mkutano wa Global Business Forum 2017 kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika, mkutano huo wa siku mbili umefanyika Dubai, UAE na kuhudhuriwa na watu 5860 wakiwepo viongozi wa serikali za nchi za Afrika na wafanyabiashara. (Picha na Clouds Media)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amepongeza uamuzi wa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kufufua viwanda ambavyo vilikuwa havifanyi kazi.
Dewji ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa Global Business Forum 2017 (GBF) kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).
Mfanyabiashara huyo ambaye anamiliki viwanda 41 alisema uamuzi aliochukua Rais Magufuli ni mzuri hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati.
Dewji alisema kampuni yake ya MeTL Group itaendelea kushirikiana na serikali na katika kipindi cha miaka kadhaa ijayo amejipanga kuhakikisha anatoa ajira kwa Watanzania 100,000 jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wa nchi na kwa wananchi..
Hivyo makala MOHAMMED DEWJI APONGEZA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KUFUFUA VIWANDA
yaani makala yote MOHAMMED DEWJI APONGEZA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KUFUFUA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MOHAMMED DEWJI APONGEZA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KUFUFUA VIWANDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mohammed-dewji-apongeza-jitihada-za.html
0 Response to "MOHAMMED DEWJI APONGEZA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KUFUFUA VIWANDA"
Post a Comment