Loading...
title : MBWEMBWE TU KAKOBE KUMBE HANA HATA AKAUNTI.
link : MBWEMBWE TU KAKOBE KUMBE HANA HATA AKAUNTI.
MBWEMBWE TU KAKOBE KUMBE HANA HATA AKAUNTI.
Na Maria Kaira MwambawahabariMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)imezitaka Taasisi Zote za kidini kufuata katiba zao ikiwa ni pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumizi,kufuatia kauli iliyotolewa na Askofu Zachary Kakobe wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship kuwa "yeye anapesa kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania".
Kufuatia kauli hiyo iliyotolewa na Askofu huyo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanya uchunguzi na kubaini usahihi wa kauli hiyo, ambapo iliweza kubaini kuwa Askofu Zachary Kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yoyote ya fedha hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere amesema kuwa uchunguzi ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti za kanisa (signatories) zilizopo katika benki ya NBC zenye jumla ya kiasi cha shilingi 8,132,100,819.00, kiasi hiki cha fedha kimetokana na sadaka, zaka na changizo ambazo zinatolewa na waumini wa kanisa tajwa hapo juu, hivyo kwa mujibu wa Sheria hakitozwi kodi.
"Kanisa lilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 20,834,843.00 ambazo zilitokana na uwekezaji katika makampuni ya kukuza mitaji" amesema
Pia Kamishina Kichere amesema Kodi hiyo imelipwa baada ya uchunguzi.ambapo Kampuni inayomilikiwa na watoto wa Askofu Zachary Kakobe ilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 37,280,030.00 ambazo zimelipwa baada ya uchunguzi. Kwa ujumla, kiasi cha kodi kilicholipwa kutokana na uchunguzi huu ni shilingi 58,114,873.00.
Aidha Kichere amesema Kanisa linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na ‘majaba’ kinyume na taratibu za utunzaji wa fedha, lakini pia uwekaji na utoaji wa fedha nyingi kutoka benki haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika" amesema
Hata hivyo
Hivyo makala MBWEMBWE TU KAKOBE KUMBE HANA HATA AKAUNTI.
yaani makala yote MBWEMBWE TU KAKOBE KUMBE HANA HATA AKAUNTI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBWEMBWE TU KAKOBE KUMBE HANA HATA AKAUNTI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mbwembwe-tu-kakobe-kumbe-hana-hata.html
0 Response to "MBWEMBWE TU KAKOBE KUMBE HANA HATA AKAUNTI."
Post a Comment