Loading...
title : MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JANUARI UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.0-NBS
link : MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JANUARI UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.0-NBS
MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JANUARI UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.0-NBS
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MFUMUKO wa bei wa Taifa wa Januari 2018 umebaki kuwa asilimia 4.0 kama ilivyokuwa mwezi Desemba 2017 kwa ujumla inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2018 imekuwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Epharaim Kwesigabo amesema kubaki kwa mfumko huo kunatokana na bidhaa na huduma kuendelea bei ileilie ya mwezi Desemba.
Amesema baadhi ya bidhaa za vyakula vilivyochangia kupungua kwa mfumuko wa bei huo ni Mahindi kwa asilimia 8.0, Maharage 4.3. Ndizi ya kupika asilimia 9.0, Samaki kwa asilimia 9.0 kwa upande mwingine baadhi ya bei za bidhaa zisizo za Chakula zilizochangia mfumuko wa bei ya mwezi Januari 2018 ni pamoja na sare za shule kwa asilimia 2.3, Huduma za afya kwenye Hospitali Binafsi kwa asilimia 10.0, Mkaa asilimia 9.4, Vitabu vya shule kwa asilimia 2.7 na gharama za malazi asilimia 3.2.
Kwesigabo amesema mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unafanana na nchi nyingine Afrika Mashariki ambapo Kenya Mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2018 umeongezeka hadi asilimia 4.83 kutoka asilimia 4.50 kwa mwaka ulioishia Desemba 2017, Uganda Mfumuko wa bei umepungua hadi kufikia asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia wa mwezi Desemba 2017.
Aidha amesema Mfumuko wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.
Kwesigabo amesema NBS ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa sheria ya kufanya uratibu upatikanaji wa takwimu rasmi.

Hivyo makala MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JANUARI UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.0-NBS
yaani makala yote MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JANUARI UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.0-NBS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JANUARI UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.0-NBS mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mfumuko-wa-bei-kwa-mwezi-januari.html
0 Response to "MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JANUARI UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.0-NBS"
Post a Comment