Loading...
title : MTANGAZAJI LIKUDA AHAMIA A.FM RADIO
link : MTANGAZAJI LIKUDA AHAMIA A.FM RADIO
MTANGAZAJI LIKUDA AHAMIA A.FM RADIO
Mtanganzaji mkongwe nchini Emmanuel Likuda,leo amejiunga rasmi na A.FM RADIO kama mtanganzaji akijikita zaidi katika kipindi cha Amka tofauti.
Akiongea wakati wakumtambulisha Likuda kwa wasikilizaji,Meneja mkuu wa A.FM Bw. Tatenda Nyawo amesema,hiyo ni zawadi maalum na upendo kwa wasikilizaji wa a.fm 92.9 Dodoma,hasa katika msimu huu wa siku kuu ya Wapendanao (VALENTINES).
Bw.Tatenda ameongeza kuwa Likuda ni mtangaji mwenye uzoefu wa kutosha katika masuala ya utangazaji,hivyo kujiunga kwake na Af.m ni njia moja wapo ya kukipeleka kitu hicho katika hatua nyingine,kama ilivyo kauli mbiu ya A.fm kwa mwaka huu ‘’2018 level Nyingine”.
Kwa upande wake Likuda amesema ni furaha sana kujiunga na A.fm na kutokana na uwezo na uzoefu alionao,ana Imani kuwa A.fm itasonga mbele Zaidi katika kutimiza dhima yake kwa jamii hasa wakazi wa Dodoma na kwamba vipo vitu vingi ambavyo amejipanga kuvitoa kama zawadi kwa wasikilizaji wa A.FM kupitia kipindi cha AMKA TOFAUTI ambacho hurushwa kila siku kuanzia JUMATATU- IJUMAA saa 11:00 Mpaka saa 03:00 Asubuhi. Meneja mkuu wa A.fm Radio Tatenda Nyawo (kushoto)akiwa kwenye picha ya pamoja na mtangazaji Emmanuel Likuda mapema leo,baada ya mtangazaji huyo kutambulishwa rasmi kwa wasikilizaji kama mtangazaji wa kipindi cha Amka Tofauti kinachorushwa na A.FM
Likuda kwenye picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha Amka Tofauti Victor Simon na Elizabeth Kachenje.
Mtangazaji Likuda akiwa na watangazaji wa kipindi cha Amka Tofauti,kushoto ni Victor Simon,Elizabeth Kachenje na msimamizi wa Vipindi Ally Mohamed (Kulia).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MTANGAZAJI LIKUDA AHAMIA A.FM RADIO
yaani makala yote MTANGAZAJI LIKUDA AHAMIA A.FM RADIO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTANGAZAJI LIKUDA AHAMIA A.FM RADIO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mtangazaji-likuda-ahamia-afm-radio_12.html
0 Response to "MTANGAZAJI LIKUDA AHAMIA A.FM RADIO"
Post a Comment