Loading...
title : SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.
link : SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.
SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.
Mwambawahabari
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeadhimia kukusanya na kutumia takwimu kwa njia ya kielektroniki nchi nzima ili kuweza kumudu na kutoa huduma za afya kwa ubora zaidi nchini.“Takwimu ni muhimu sana ambazo zitazomuwezesha mtoa huduma kujua mgonjwa historia yake ya ugonjwa na matibabu aliyopewa awali,kuwapa Uwezo utumishi kujua tunahitaji rasilimali watu kwa kiasi gani katika kituo cha Afya” alisema Dkt. Ulisubsya.
Aidha, Dkt. Ulisubisya amesema kuwa zoezi hilo litaanza kwenye mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Manyara hatimaye kufikia nchi nzima mpaka kufika 2020 ili kuweza kuwa na takwimu za afya.
Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mfumo wa kujaza takwimu kwenye makaratasi umepitwa na wakati kwani kadri makaratasi ya takwimu yanavyokuwa mengi na makosa ya utoaji huduma yanaweza kutokea kwani mpaka uanze kutafuta takwimu zilizopita inachukua muda mrefu tofauti na kuhifadhi takwimu kielektroniki.
Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mpaka hivi sasa hali ya utoaji wa chanjo imefikia asilimia 97 na lengo letu ni kufikia asilimia 100 kupitia mfumo huu wa kukusanya takwimu kwa njia ya kielektroniki.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Matthieu Kamwa amesema kuwa wapo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika kutekeleza hilo ili kuweza kuboresha mifumo ya afya nchini.
“Unajua Takwimu ni utajiri hasa katika kutekeleza shughuli za kutoa huduma za afya kwa wananchi hivyo hatuna budi kuunga mkono juhudu za Serikali ya Tanzania katika kufanikisha jambo hili kwani litaturahisishia hata sisi katika kutoa miongozo ya afya” alisema Dkt. Kamwa.
Hivyo makala SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.
yaani makala yote SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/serikali-yaadhimia-kukusanya-takwimu-za.html
0 Response to "SERIKALI YAADHIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA."
Post a Comment