Loading...
title : WAHAMIAJI WALOWEZI WATAKIWA KUFIKA OFISI ZA UHAMIAJI –IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA DAR ES SALAAM
link : WAHAMIAJI WALOWEZI WATAKIWA KUFIKA OFISI ZA UHAMIAJI –IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA DAR ES SALAAM
WAHAMIAJI WALOWEZI WATAKIWA KUFIKA OFISI ZA UHAMIAJI –IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA DAR ES SALAAM
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewasaa wahamiaji walowezi kujiorodheshwa katika ofisi za uhamiaji za wilaya baada ya kufanya hivyo watapewa vibali ya ukaazi vitavyofanya kuishi nchini kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Petro Malima amesema kuwa uandikishaji wahamiaji walowezi ni la nchi nzima hivyo kwa wahamiaji walowezi lazima wajiorodheshe kwa kuwa na picha tatu za Passport zilizo katika wakati na wenye watoto wanatakiwa kuwa na picha tatu hizo.
Amesema kuwa kwa wale wataofanya hivyo watatambulika na kuendelea kuishi nchini bila kusumbuliwa kuhusu masuala ya uhamiaji na kutofautisha na wakimbizi na wahamiaji haramu.
Malima amesema wageni wote wanatakiwa kuitikia wito huo wa serikali pamoja na wale ambao sio na wanaishi kufanyakazi au biashara kinyume na sheria za nchi wanatakiwa kufika katika ofisi za wilaya za kuhalalisha ukaazi na kupewa vibali vinavyostahili kwa mujibu wa sheria za nchi.
Amesema kuwa yeyote atakayejificha katika zoezi hilo na baadaye kubainika anaishi kinyume cha cha sheria hatua kali zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufukuzwa nchini mara moja au kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kukiuka sheria.
Aidha Malima amesema kuwa kuna matapeli ambao wamekuwa wakiwasumbua wageni wanaoingia nchini kwa kudai kuwa wao ni askari au maafisa wa uhamiaji na wakiwa hawana hata sare na kuwataka wanaowafanyia hivyo kudai vitambulisho na wakishindwa kufanya hivyo kuwaripoti katika vituo vya polisi vilivyo karibu.
“Viongozi wetu wanajitahidi kwa kila hali kuitangaza nchi yetu na kuvutia wawekezaji sisi uhamiaji Dar es Salaam hatuwezi kukaa kimya na kuona hii ni nia njema ya serikali inaharibu na watu wachache wasiotakia mema nchi yetu .tukumbuke wawekezaji na wataalam wa kigeni wanatakiwa nan chi zingine zinazotuzunguka , sasa hatuwezi kupoteza nafasi hiyo kwa wageni kusema kuwa Tanzania siyo sehemu sahihi ya kuwekeza kwa sababu ya usumbufu wanaoupata tutambana na kila atakayejaribu kuharibu sifa ya nchi yetu”amesema Malima.
Naibu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Petro Malima akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na wahamiaji walowezi kujisajili ili kuweza kupatiwa vibali vya kuishi nchini , leo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala WAHAMIAJI WALOWEZI WATAKIWA KUFIKA OFISI ZA UHAMIAJI –IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA DAR ES SALAAM
yaani makala yote WAHAMIAJI WALOWEZI WATAKIWA KUFIKA OFISI ZA UHAMIAJI –IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAHAMIAJI WALOWEZI WATAKIWA KUFIKA OFISI ZA UHAMIAJI –IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA DAR ES SALAAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/wahamiaji-walowezi-watakiwa-kufika.html
0 Response to "WAHAMIAJI WALOWEZI WATAKIWA KUFIKA OFISI ZA UHAMIAJI –IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA DAR ES SALAAM"
Post a Comment