Loading...
title : WAAJIRI WANAOTUHUMIWA KUTOJISAJILI MFUKO WA FIDIA KORTINI
link : WAAJIRI WANAOTUHUMIWA KUTOJISAJILI MFUKO WA FIDIA KORTINI
WAAJIRI WANAOTUHUMIWA KUTOJISAJILI MFUKO WA FIDIA KORTINI
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WAAJIRI wa kampuni nne tofauti wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa kadhaa yakiwemo ya kushindwa kujisajili na kuwasilisha taarifa za shughuli wanazozifanya kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi [WCF].
Washtakiwa hao, Malakkara Semis na Shafeek M. Purayil ni Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya SPASH INTENATIONAL CO. LTD. Silas Shemdoe na Deusdedit Samwel Kibassa ambao ni Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya ENCC CONSULTANTS.
Wengine ni Wakurugenzi Watendaji wa LASAR LOGISTIC, Abshir Farah Gure na Farhiya Hersiwarsame, wakati Mshtakiwa mwingine ni Josephat Alexander ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KAMANDA SECURITY GUARDS CO. LTD.
Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao na waendesha mashtaka tofauti wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Emilly Kiria mbele ya Hakimu Mfawidhi Victoria Nongwa. Wanashtakiwa kinyume cha Kifungu cha 71 (1) (a) na 71 (4) cha Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi Sura ya 263 marejeo ya mwaka 2015.
Akisoma mashtaka yanayomkabili Joseph inadaiwa Januari, mwaka 2018 walishindwa kujisajili na kutoa taarifa muhimu za shughuli zake na za wafanyakazi kwa Ofisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Ilidaiwa Januari 11, mwaka 2018 mshtakiwa huyo alishindwa kutoa taarifa mihimu za waajiriwa wake ikiwamo majina na mishahara ya wafanyakazi.
Katika kesi ya jinai namba 33 ya mwaka 2018, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benson Mangowi alidai washtakiwa Malakhara Semis na Shafeek Purayil wa kampuni ya Spash International Co.Ltd Desemba 25,mwaka 2017 walishindwa kusajili na kutoka taarifa muhimu za shughuli za kampuni kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya Spash International Co Ltd Shafeek Purayil (kulia) na Japhet Alexander wa Kampuni ya Kamanda Security Guard Co. Ltd, wakipelekwa mahabusu ya Mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 2018 baada ya kusomewa mashtaka mawili ya jinai kwa kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), na kuwasilisha taarifa za shughuli za Makampuni wanayoyaongoza kwa Mfuko huo. Washtakiwa wakipatikana na hatia wanakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka mitano (5), jela au faini isiyozidi shilingi milioni hamsini au vyote kwa pamoja.
Shafeek Purayil(mbele) na Japhet Alexander wakitoka mahakamani baada ya kusomewa mashtaka na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Bibi Victoria Nongwa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAAJIRI WANAOTUHUMIWA KUTOJISAJILI MFUKO WA FIDIA KORTINI
yaani makala yote WAAJIRI WANAOTUHUMIWA KUTOJISAJILI MFUKO WA FIDIA KORTINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAAJIRI WANAOTUHUMIWA KUTOJISAJILI MFUKO WA FIDIA KORTINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/waajiri-wanaotuhumiwa-kutojisajili.html
0 Response to "WAAJIRI WANAOTUHUMIWA KUTOJISAJILI MFUKO WA FIDIA KORTINI"
Post a Comment