Loading...

TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI

Loading...
TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI
link : TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI

soma pia


TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani (2017 Democracy Index) iliyozinduliwa Februari 2, mwaka huu na kuchapishwa na jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist imeitaja Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika maswala ya Utawala Bora kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alisema kuwa Tanzania kuwa nchi ya kwanza kwenye masuala ya Utawala bora imeweza kusaidia ukuaji wa Uchumi wake.

“Utawala Bora ni kigezo muhimu cha ukuaji wa uchumi na hata ustawi wa jamii, kama ambavyo Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani iliyotolewa na jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist imeitaja Tanzania ni ya kwanza katika ukanda wa EAC, ikifuatiwa na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC. 

Pia, ripoti ya Foresight Afrika na taarifa ya Uchumi ya Benki ya Dunia vyote vimeitaja Tanzania kuwa katika nchi tano Bora za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi katika mwaka 2018, nchi hizo ni Ghana, Ethiopia, Kodivaa , Senegali na Tanzania”.

Aidha, Dkt. Abbasi alisema kuwa ukuaji huo wa uchumi ni dhamira isiyoyumba ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uchumi mkuu unaendelea kujiakisi katika maisha ya watanzania kupitia utoaji wa huduma kwa wananchi na kuboresha sekta mbalimbali.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi mbalimbali za Serikali mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi mbalimbali za Serikali mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo



Hivyo makala TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI

yaani makala yote TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/tanzania-kinara-utawala-bora-afrika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANZANIA KINARA UTAWALA BORA AFRIKA MASHARIKI"

Post a Comment

Loading...