Loading...
title : Zaidi ya Bilioni 25 kutekeleza shughuli mbalimbali Halmashauri Wilaya Njombe
link : Zaidi ya Bilioni 25 kutekeleza shughuli mbalimbali Halmashauri Wilaya Njombe
Zaidi ya Bilioni 25 kutekeleza shughuli mbalimbali Halmashauri Wilaya Njombe
Na Lukelo Mshaura- Njombe.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Njombe limepitisha mapendekezo ya rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 wilayani hapa.
Katika mapendekezo hayo baraza hilo limepitisha kiasi cha zaidi ya bilioni 25.2 kutumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.
Akisoma mpango na rasimu ya bajeti kwenye kikao cha baraza la madiwani ,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Bi Monica Kwiluhya alivitaja vyanzo vya kufanikisha bajeti hiyo kuwa ni Serikali Kuu, wafadhili, mapato ya ndani, uchangiaji wa huduma za afya, uchangiaji wa ada kidato cha tano na sita pamoja na mchango wa jamii kwenye miradi ya maendeleo.
Akiainisha mchanganuo wa vyanzo hivyo Bi Kwiluhya alibainisha kuwa Serikali kuu inatarajiwa kuchangia kiasi cha bilioni 20.179, wafadhili bilioni 2.965, mapato ya ndani halisi bilioni 1,439, uchangiaji huduma za afya zaidi ya milioni 140, uchangiaji ada ya kidato cha tano na sita milioni 42 huku mchango wa jamii kwenye miradi ya maendeleo ukiwa ni kiasi cha milioni 520.
Bi kwiluhya alifafanua kuwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya wilaya ya Njombe imekadiria kutumia zaidi ya bilioni tano ( 5) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Bi Monica Kwiluhya akiwasilisha mapendekezo ya mpango na bajeti wa Halmshauri ya wilaya ya Njombe wa mwaka 2018/2019.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe wakifuatilia mjadala wa mapendekezo ya bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka wa fedha 2018/2019.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Zaidi ya Bilioni 25 kutekeleza shughuli mbalimbali Halmashauri Wilaya Njombe
yaani makala yote Zaidi ya Bilioni 25 kutekeleza shughuli mbalimbali Halmashauri Wilaya Njombe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Zaidi ya Bilioni 25 kutekeleza shughuli mbalimbali Halmashauri Wilaya Njombe mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/zaidi-ya-bilioni-25-kutekeleza-shughuli.html
0 Response to "Zaidi ya Bilioni 25 kutekeleza shughuli mbalimbali Halmashauri Wilaya Njombe"
Post a Comment