Loading...
title : 17 WATAMBULIWA KATI YA 26 WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKURANGA
link : 17 WATAMBULIWA KATI YA 26 WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKURANGA
17 WATAMBULIWA KATI YA 26 WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKURANGA
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
WATU 17 kati ya 26 waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea Mkuranga Mkoani Pwani ,wametambuliwa majina yao ambapo hatua inayoendelea ni kuwakabidhi kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi. Aidha watu wengine 10 waliojeruhiwa walikimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga, Stephen Mwandambo alisema amepokea maiti 25 na majeruhi hao ambapo majeruhi mmoja alifariki njiani wakati wakipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mganga mkuu huyo aliwataja waliofariki na kutambuliwa majina yao ni 17 kati ya 26 waliofariki kuwa ni pamoja na Selemani Guli (36) mkazi wa Kongowe,Modesta Sheleli (24 ) mkazi wa Vianzi,Doreen Selemani Seleli (5), sheila Hamad Mkuba ( 8 )mkazi wa Vianzi na Mariam Hussein Sadik (15 )mkazi wa Mwarusembe.
Wengine aliotaja ni Nassoro Hamis( 48) mkazi wa Jaribu Mpakani, Asha Athumani (24)mkazi wa Songosongo ,Nasma Athuman 22 Songosongo Mwanahawa Athuman (52),Mohammed Saidi (25) mkazi wa Njopeka na Mwajabu Jongo (20)mkazi wa Njopeka";
Dokta Mwandambo aliwataja marehemu wengine kuwa ni Mwarami Mbunju(37) mkazi wa Mkamba na Abisaalom Uloga (25)mkazi wa Kimanzichana ,Kijongo Kibwana Jongo(26 )anakaa Jaribu Mpakani na Recho Japhet (16),Mariam Selemani (36)mkazi wa Mbagala na Melania Kapatwa (38)mkazi wa Jaribu Mpakani.

Kaimu kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Kibiti Mohammed Likwata akithibitisha anesena ajali imetokea usiku wa kuamkia machi 25 mwaka huu katika eneo la Kitonga kata ya Mwalusembe wilaya ya humo.
Chanzo cha ajali inadaiwa mwendo kasi wa dereva wa lori katika kilima na kusababisha ajali hiyo mbaya. Simanzi zimetawala katika wilaya hiyo ,ambapo mbunge wa jimbo la Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega aliishukuru serikali ya wilaya chini ya mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kwa juhudi zake za kusaidia majeruhi na marehemu kupelekwa hospitalini.
Mhe. Ulega alitoa pole kwa wafiwa na majeruhi na kuwaasa madereva waache kuendesha kwa mwendo kasi kwani husababisha ajali zembe. "Naishukuru pia hospitali ya wilaya kwa juhudi zao baada ya kupokea marehemu na majeruhi kuhangaikia kuokoa maisha yao." alieleza Ulega.
Hivyo makala 17 WATAMBULIWA KATI YA 26 WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKURANGA
yaani makala yote 17 WATAMBULIWA KATI YA 26 WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKURANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala 17 WATAMBULIWA KATI YA 26 WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKURANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/17-watambuliwa-kati-ya-26-waliofariki.html
0 Response to "17 WATAMBULIWA KATI YA 26 WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKURANGA"
Post a Comment