Loading...

BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO

Loading...
BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO
link : BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO

soma pia


BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO

Na Rhoda Ezekieli, Kigoma

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wameikataa miradi minne ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni mbili iliyoanza kutekelezwa tangu mwaka 2012.

Miradi hiyo inafadhiliwa na Benki Kuu ya Dunia na ikiwa chini ya uangalizi wa Wilaya ya Kibondo ambayo mpaka sasa bado haijakamilika.

Madiwani hao wameitaja miradi hiyo ni wa maji Nyagwijima, Kiduduye, Katanga na Muhange ambayo imetekelezwa kwa muda mrefu licha ya fedha zote zilishatolewa lakini haikamiliki na sasa wamechoka kupewa majibu ya kuahidiwa kila kukicha.
Wakizungumza jana katika kikao cha baraza hilo, madiwani hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipewa majibu ambayo hayaeleweki huku wakiahidiwa miradi hiyo itakamilika ndani ya mwezi mmoja baada ya kikao cha baraza la madiwani na mpaka sasa kimekuwa kitendawili kisicho na majibu.

Diwani wa Kata ya Gwarama Elia Kanjero amesema imekuwa kama desturi kupewa majibu mepesi katika suala hilo na hawataendelea kuona miradi hiyo ikionekana kuwepo katika maeneo yao bila faida yoyote kwa wananchi.

Alisema ni aibu miradi hiyo hata wafadhili wakija kuiangalia wanaweza kuacha kutoa fedha zao katika miradi mingine."Miradi hii inaonesha kutokuwa na tija kwa wananchi na haifai kabisa kutokana na fedha zilizotumika na ukizingatia fedha zote zimekwishalipwa lakini miradi ni mibovu," amesema.
Aidha Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ambaye kwenye baraza hilo alikaimu nafasi Mwenyekiti, Toy Butono amesema baraza linapendekeza Mhandisi wa Maji wilaya hiyo avuliwe madaraka yake.Pia achunguzwe kutokana na kushindwa kufuatilia miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa adhabu nyingine ili kukomesha uzembe kwa watumishi unaoweza kuigharimu halmashauri.

"Baraza tunaikataa miradi hii na tunaomba Mhandisi wa Maji anyang'anywe madaraka kwa kipindi hiki apewe mtu mwingine, yeye kazi hii imemshinda kila siku tunapokea malalamiko kutoka kwa wananchi." Kuhusu miradi hiyo kwa sasa hatuihitaji hadi itakapo kamilika na Mhandisi atuambie labda alishiriki kufanya miradi hiyo isikamilike kwanini ashindwe kufuatilia", amesema Butono.

Mbunge wa jimbo la Buyungu Kasuku Bilago amesema suala hilo atalifikisha Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) ili hatua zichukuliwe kwa wanaokwamisha miradi hiyo ambayo ni muhimu kwa wananchi.

"Wapo baadhi ya wananchi waliochangia nguvu zao bila kupewa haki zao mpaka sasa na kuwapongeza madiwani kwa uamuzi mgumu waliouchukua," amesema.Kwa upande wake Ofisa Utumishi wa halmashauri hiyo , Lusajo Ngabo ametoa ushauri kuhusu uamuzi uliochukuliwa na kuomba nhusika apewe siku 18 ili ajitetee kuhusu tuhuma zinazomkabili na baada ya hapo sasa ndio hatua nyingine zifuatwe.


Hivyo makala BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO

yaani makala yote BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/baraza-la-madiwani-waikataa-miradi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BARAZA LA MADIWANI WAIKATAA MIRADI MINNE YA MAJI KAKONKO"

Post a Comment

Loading...