Loading...
title : KAMPUNI YAJITOSA KUSAKA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
link : KAMPUNI YAJITOSA KUSAKA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
KAMPUNI YAJITOSA KUSAKA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya Carrer Times Ltd inayoshighulisha na teknolojia imeandaa Africa Technology Awards yenye lengo la kusaka na kuibua wabunifu katika mambo yanayohusu teknolojia na hasa ya habari na mawasiliano nchini.
Imesema kuna vijana wengi ambao wanao uwezo wa kubuni mambo yanayoweza kusaidia maendeleo ya nchi, hivyo wameamua kuchukua jukumu hilo kwa kutoa tuzo hiyo baada ya kushindanisha kazi za ubunifu ambazo washiriki watazionesha kwao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Carrer Time Ltd Hawa Hongo amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa watatoa tuzo hiyo baada ya kupata washindi kwenye mambo ya ubunifu na kuanzia kesho wataanza kutoa fomu kwa wanaotaka kushiriki.
"Tunafahamu kuna vijana wengi ambao wapo mtaani na wanao uwezo mkubwa katika kubuni mambo yanayohusu teknolojia na hao ndio ambao tunawataka kuwaibua kwa maslahi ya nchi yetu.Tunaka vijana ambao wataoesha uwezo wao halisi katika mambo ya ubunifu,"amesema.
Amesema kumekuwepo na mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yakiibua vipaji lakini kwenye mambo ya ubunifu katika mambo yanayohusu teknolojia haifanyiki sana na hivyo wao kupitia kampuni yao wameamua kusaka vijapaji vilivyojificha mtaani.
Kuhusu taratibu za kupata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano hayo, amesema wataanza kutoa fumu ambazo zitakazokuwa zinatolewa kwenye ofisi zao zilizopo Mikocheni B mtaa wa Huruma jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Carrier Time Ltd, Hawa Hongo akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari alipokuwa anazungumzia Africa Teknology Awards 2018 itakayotolewa na kampuni yao Mei mwaka huu kwa washindi wa shindano la ubunifu katika mambo ya teknolojia
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala KAMPUNI YAJITOSA KUSAKA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
yaani makala yote KAMPUNI YAJITOSA KUSAKA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YAJITOSA KUSAKA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/kampuni-yajitosa-kusaka-wabunifu-wa.html
0 Response to "KAMPUNI YAJITOSA KUSAKA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO"
Post a Comment