Loading...
title : KASI YA MADIWANI JIMBONI KWA MCHUNGAJI MSIGWA KUJIUZULU INATISHA , YUPO KATIBU WA CHADEMA MKOA
link : KASI YA MADIWANI JIMBONI KWA MCHUNGAJI MSIGWA KUJIUZULU INATISHA , YUPO KATIBU WA CHADEMA MKOA
KASI YA MADIWANI JIMBONI KWA MCHUNGAJI MSIGWA KUJIUZULU INATISHA , YUPO KATIBU WA CHADEMA MKOA
Katibu wa Chadema mkoa wa Iringa Oscar Ndale katikati akiwa na diwani wa Mwangata Anjelus Mbogo na katibu kata ya Mwangata Tumaini Gwivaha baada ya kujiuzulu leo
Na MatukiodaimaBlog.
IDADI ya madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) jimbo la Iringa mjini kujiuzulu imezidi kuongezeka na kufikia madiwani saba sasa baada ya watatu kujiuzulu ndani ya wiki hii pamoja na katibu wa chadema mkoa wa Iringa Oscar Ndale .
wakati diwani wa Kwakilosa na Ruaha walijiuzulu kwa pamoja juzi diwani wa Mwangata Anjelus Mbogo alijiuzulu leo pamoja na katibu wa mkoa wa chama hicho na katibu kata wa Chadema Mwangata Tumaini Gwivaha .
wakitangaza azma ya kujiuzulu kwao nafasi hiyo mbele ya waandishi wa habari Mbogo na Ndale walisema kuwa kujiuzulu kwao kumetokana na mahusiano mabaya ya kufifisha maendeleo kwenye kata yake pamoja na mabavu ya viongozi w juu wa Chadema .
kati yake na viongozi wa juu wa Chadema hicho akiwemo mwenyekiti wa kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ambae ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini pamoja na uongozi wa juu wa Chadema ukiongozwa na mwenyekiti wake Taifa Freeman Mbowe.
" Vyama vya siasa vipo vingi kuna CUF , ACT Wazalendo na CCM hivyo nitachagua ni chama gani kitanifaa kufanya siasa zangu ila hata CCM nipo tayari hakuna ubaya "
Alisema kuwa mbunge Msigwa amekuwa akimfanyia diwani mwenzao Joseph Lyata figisu figisu toka akiwa naibu meya wa Manispaa ya Iringa na hofu ya mbunge Msigwa ni baada ya kuhisi kuwa anautafuta ubunge wa jimbo hilo mwaka 2020 .
Diwani Mbogo alisema kwa sasa atabaki mwanasiasa huru na iwapo mbunge Msigwa na mstahiki meya Alex Kimbe wataondoka hata leo chadema basi atarejea Chadema ila kama wataendelea kubaki hatarudi kamwe .
Kwa upande wake aliyekuwa katibu wa Chadema mkoa ,Ndale alisema kuwa kuyumba kwa chadema Iringa mjini kumesababishwa na mbunge kutokuwa na ushirikiano mzuri na wenzake na mara kadhaa wamekuwa wakimuonya ila bado anaendelea na kuwa Mbowe pia amesababisha kujiuzulu kwake nafasi hiyo na kwa sasa atajiunga na CCM .
Ndale alisema aliomba kujiunga na CCM na amekubaliwa na hivyo ataendelea na Siasa kupitia CCM huku akisema uhai wa Chadema Iringa mjini umefika mwisho .
Kwa upande wake Joseph Lyata aliyekuwa diwani kata ya Kwakilosa alisema siasa ndani ya Chadema kwake imemshinda hivyo ameamua kuondoka ndani ya chama hicho na kuwa mwanasiasa huru .
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini Omary Mkangama ambae ni kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa amethibitisha kupokea barua za madiwani watatu ndani ya wiki hii kutoka Chadema ambao wamejiuzulu nafasi zao Tandesy Sanga wa kata ya Ruaha , Joseph Lyata kata ya Kwakilosa na Anjelus Mbogo wa kata ya Mwangata .
" Kwa mujibu wa sheria nitamuandikia barua mstahiki meya ili yeye aweze kumwandikia waziri mwenye dhamana ambae ataijulisha tume wa Taifa ya uchaguzi ili taratibu nyingine zifanyike "
Alisema jimbo la Iringa linazo kata 18 kati ya madiwani hao CCM ina madiwani watano pamoja na yule wa Kihesa aliyepita bila kupingwa itakuwa na madiwani sita huku Chadema itabaki na madiwani 9.
Hivyo makala KASI YA MADIWANI JIMBONI KWA MCHUNGAJI MSIGWA KUJIUZULU INATISHA , YUPO KATIBU WA CHADEMA MKOA
yaani makala yote KASI YA MADIWANI JIMBONI KWA MCHUNGAJI MSIGWA KUJIUZULU INATISHA , YUPO KATIBU WA CHADEMA MKOA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KASI YA MADIWANI JIMBONI KWA MCHUNGAJI MSIGWA KUJIUZULU INATISHA , YUPO KATIBU WA CHADEMA MKOA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/kasi-ya-madiwani-jimboni-kwa-mchungaji.html
0 Response to "KASI YA MADIWANI JIMBONI KWA MCHUNGAJI MSIGWA KUJIUZULU INATISHA , YUPO KATIBU WA CHADEMA MKOA"
Post a Comment