Loading...
title : 'KWA MARA YA KWANZA MAMLAKA HALI YA HEWA WAMETABIRI UKWELI KUHUSU MVUA'
link : 'KWA MARA YA KWANZA MAMLAKA HALI YA HEWA WAMETABIRI UKWELI KUHUSU MVUA'
'KWA MARA YA KWANZA MAMLAKA HALI YA HEWA WAMETABIRI UKWELI KUHUSU MVUA'
Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii
KWA mara ya kwanza wamepatia!Ndivyo ambavyo kwa siku ya leo
baadhi ya wananchi hasa wa Jiji la Dar es Salaam wanavyodai baada
ya mvua kunyesha kama ambavyo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA )ilivyotabiri.
Kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakidhani TMA wamekuwa wakibahatisha kwenye tabiri zao hasa pale inapotokea walitabiri mvua kunyesha katika eneo fulani halafu mvua hainyeshi na kusababisha maswali.
Siku za hivi karibuni, TMA ilitoa taarifa kwa umma kuwa mwanzo mwa Machi mwaka huu mvua zitaanza kunyesha na kuomba wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari mapema ili kuepuka athari za mvua.
Hivyo kitendo cha mvua kunyesha leo jijini Dar es Salaam ambayo ni mwanzoni mwa Machi , wananchi ambao wamezungumza na Michuzi Blog wamedai ni kwa mara ya kwanza Mamalaka ya Hali Tanzania imetabiri kwa usahihi na kuwataka kuendelea kutoa tabiri ambazo zinaendena na ukweli ili kuendelea kuaminika.
Mshana John ambaye ni mkazi wa Kigamboni ametoa pongezi kwa TMA huku akidai alikuwa anasubiri ka hamu Machi ifike ili aone kama utabiri kuhusu mvua ulikuwa wenye ukweli lakini sasa ameamini na kusisitiza kwake ni mara ya kwanza kuona kilichotabiriwa kinakwenda na wakati.
"Niwe kweli nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa taarifa kuhusu hali ya hewa, ila kuna wakati wanatabiri kuwa mvua itanyesha lakini matokeo yake hakuna mvua na jua linabaki kuwa kali.Ila kwa mara ya kwanza wamepatia lazima tuwapongeze kwa kazi nzuri wanayoifanya.
"Huenda sasa watakuwa wamejiimarisha kwa kuwa na vifaa ambavyo vinakwenda na taarifa sahihi na ndio maana wametabiri uhalisia .Walisema mvua itanyesha mwanzoni mwa Machi na leo ndio mwanzo wenyewe na kweli imenyesha,"amesema John.

Hivyo makala 'KWA MARA YA KWANZA MAMLAKA HALI YA HEWA WAMETABIRI UKWELI KUHUSU MVUA'
yaani makala yote 'KWA MARA YA KWANZA MAMLAKA HALI YA HEWA WAMETABIRI UKWELI KUHUSU MVUA' Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala 'KWA MARA YA KWANZA MAMLAKA HALI YA HEWA WAMETABIRI UKWELI KUHUSU MVUA' mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/kwa-mara-ya-kwanza-mamlaka-hali-ya-hewa.html
0 Response to "'KWA MARA YA KWANZA MAMLAKA HALI YA HEWA WAMETABIRI UKWELI KUHUSU MVUA'"
Post a Comment