Loading...

MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI

Loading...
MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI
link : MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI

soma pia


MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

DAKTARI Bingwa mwandamizi wa upasuaji mifupa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI), Paul Marealle amesema tayari wamemfanyia upasuaji Martha Malambi (25)ambaye amenusurika kufa baada ya kupambana na mamba katika mto Mgeta uliopo Dakawa mkoani Morogoro.

Martha alifikishwa MOI kwa ajili ya matibabu zaidi kabla ya kufanyiwa upasuaji huo leo asubuhi, alianza kupatiwa matibabu mengine ya kutibu majereha yaliyopo mwilini yaliyotokana na meno ya mamba wakati anapambana kuokoa maisha yake.

Akizungumza na Michuzi Blogu leo, Dk.Marealle amesema tayari Martha amefanyiwa upasuaji na sasa anaendelea vizuri.

Dk. Marealle amesema Martha alipata jeraha kubwa la kuvunjika mfupa wa paja la mguu wa kulia,hivyo pamoja na tiba nyingine wamemfanyia upasuaji na kumuwekea chuma ndani ya paja.

"Mgonjwa anaendelea vizuri , tumefanikiwa kumfanyia upasuaji na amerudishwa wodini kwa ajili ya mapumziko na uangalizi zaidi.Kwa kuwa upasuaji umefanyika ataruhusiwa ndani ya siku mbili hizi,"amesema Dk.Marealle.

Martha ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Ukutu huko Dakawa mkoani Morogoro,akielezea tukio hilo kwa kifupi anasema kinachomuuma zaidi mbali ya yeye kujeruhiwa ni mtoto wake wa mwaka mmoja Godfrey David amefariki wakati wa tukio hilo na maiti yake imesombwa na maji.

Amesema akiwa mtoni alikoenda kuteka maji, wakati anajiandaa kuondoka mtoni, ghafla alitokea mamba mkubwa na kisha kuvuta mguu na kumtupia kwenye kina kirefu cha maji.

Wakati anahangaika kujiokoa ndipo mtoto wake alipokunywa maji mengi na kumsababisha kifo na maiti yake imesombwa na maji. Kwani alikuwa amembeba mgongoni na hivyo kanga ilifunguka na mtoto kwenda na maji.



Hivyo makala MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI

yaani makala yote MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mama-aliyenusurika-kuliwa-na-mamba.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAMA ALIYENUSURIKA KULIWA NA MAMBA MTONI AFANYIWA UPASUAJI MOI"

Post a Comment

Loading...