Loading...

MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE

Loading...
MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE
link : MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE

soma pia


MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE

Gari la Jeshi la Polisi lilipowasili katika Maahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam likiwa na Dk.Mashinji, Mnyika, Msigwa na Ester Matiko.

*Yumo pia Dk.Mashinji, Mnyika, Msigwa na Ester Matiko

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe na vingozi wenzake watano wa chama hicho wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka nane yakiwemo ya uchochezi na uasi.

Mbali na Mbowe wahtakiwa wengine ni wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Bara Salum Salum, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent Mashinji.

Katika mashtaka hayo nane, shtaka la kwanza na la pili linawakabili watuhumiwa wote sita, huku Mbowe peke yake anakabiliwa na mashtaka matano, yaani shtaka la tatu hadi la saba na Msigwa akikabiliwa na shtaka moja la peke yake la nane.

Akisoma  hati ya mashitaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Faraja Nchimbi amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa Februari 16, mwaka huu washtakiwa kwa pamoja, wakiwa katika barabara ya Kawawa wilayani Kinondoni, walifanya mkusanyiko na maandamano isivyo halali kinyume na sheria. 

Imedaiwa walikusanyika kutekeleza lengo la pamoja kufanya mkusanyiko usio wa halali wenye vurugu na kufanya watu waogope kwamba watakwenda kusababisha uvunjifu wa amani.

Aidha Nchimbi ameongeza kudai Februari 16, mwaka huu katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa wamekusanyika wao na wenzao 12 ambao bado hawajafikishwa mahakamani, wakiwa kwenye maandamano hayo,licha ya kutolewa  tamko la kuwataka kutawanyika...

Waligoma kutii amri hiyo na kuendelea na maandamano na kusababisha kifo cha Aquilina Akwkilina kusababisha askari wawili kujeruhiwa kutokana na mkusanyiko  huo.

Katika shtaka la tatu imedaiwa Februari 16, mwaka huu katika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, jijini mshtakiwa Mbowe peke yake wakati akihutubia wananchi wa jimbo hilo alihamasisha chuki isivyohalali kwa kutoa matamshi ya kuhamasisha chuki maneno ambayo yalipelekea chuki mioyoni mwa wana jamii wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Mbowe anadaiwa kufanya uchochezi na kusababisha chuki miongoni mwa wanajamii ya watanzania kinyume na sheria.
Aidha Nchimbi amedai
Katika mashitaka ya uchochezi wa uasi yanayomkabili Mbowe, inadaiwa katika maeneo hayo akiwa katika mkutano wa hadhara, 

Akiwa na nia ya kupandikiza chuki na dharau kwa watanzania dhidi ya uongozi wa kiserikali  uliopo madarakani kisheria, alitamka maneno yenye kupandikiza chuki na kuleta ushawishi wa uasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani kisheria.

Nchimbi aliendelea kudai, katika tarehe hiyo hiyo na maeneo hayo mkoani Dar es Salaam, Mbowe alitoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau dhidi ya mamlaka halali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Katika shitaka la saba, Mbowe anakabiliwa na tuhuma za kutenda kosa la kushawishi kutendeka kwa kosa la jinai, ambapo amedaiwa siku hiyo, akiwa pia amejumuika na wengine ambao hawako mahakamani, aliwashawishi wakazi hao wa Kinondoni, kutenda kosa la kufanya maandamano na mkusanyiko usio wa halali.

Mshtakia Msigwa anadaiwa kushawishi raia  kutenda kosa la jinai shtaka analodaiwa kutenda February 16, mwaka huu katika maeneo hayo hayo ya Viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni Dar es Salaam,

Imedaiwa siku hiyo Msigwa aliwashawishi wananchi wa Kinondoni kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha.

Washitakiwa wamekana mashitaka hayo na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo wanaomba ipangwe kesho au keshokutwa kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.


Hivyo makala MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE

yaani makala yote MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mbowe-wenzake-watano-wapandishwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE"

Post a Comment

Loading...