Loading...
title : Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri zaanza kupata umeme wa Gridi
link : Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri zaanza kupata umeme wa Gridi
Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri zaanza kupata umeme wa Gridi
Na Greyson Mwase, Pwani
Wilaya za Mkuranga, Kibiti na wilaya ya Rufiji katika kata ya Ikwiriri zimeanza kupata nishati ya uhakika ya umeme mara baada ya kuunganishwa katika Gridi ya Taifa na kukamilika kwa kituo cha kupozea umeme cha Mbagala kilichopo jijini Dar es Salaam.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wakati akizungumza na wananchi wa Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani katika ziara yake ya siku moja jana (tarehe 22 Machi, 2018) ya kukagua miundombinu ya umeme iliyounganishwa na Gridi ya Taifa kutokea katika kituo cha kupoza umeme cha Mbagala hadi Ikwiriri na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Dkt. Kalemani alisema lengo la kuunganisha wilaya hizo na Gridi ya taifa ni kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya umeme wa uhakika na kuondokana na umeme unaotokana na mitambo ya mafuta ya Somangafungu ambayo imekuwa ikiharibika mara kwa mara.
Alisema awali kabla ya wilaya hizo kuunganishwa na Gridi ya Taifa, kulikuwepo na changamoto ya kukatika kwa umeme katika wilaya hizo kutokana na mitambo kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara.
Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali iliamua kuunganisha wilaya hizo kwenye Gridi ya Taifa ili kuwepo na umeme wa uhakika ambao mbali na matumizi ya majumbani unategemewa na viwanda vilivyopo katika mkoa wa Pwani
Katika hatua nyingine akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kinyanya kilichopo katika wilaya ya Kibiti mkoani Pwani ambapo aliwasha rasmi umeme, Waziri Kalemani aliwataka wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kupitia REA kuhakikisha vijiji vyote na vitongoji vyake vinapata umeme wa uhakika.
Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke, Mhandisi Alex Adam (wa pili kushoto) akielezea shughuli zinazofanywa na kituo cha kupoza umeme cha Mbagala kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) katika ziara hiyo.
Mafundi wa kampuni ya Sengerema Engineering wakikamilisha ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa ajili ya kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa katika kijiji cha Kinyanya kilichopo wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akibonyeza kitufe kuashiria uwashaji wa umeme katika kijiji cha Kinyanya kilichopo wilayani Kibiti mkoani Pwani.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri zaanza kupata umeme wa Gridi
yaani makala yote Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri zaanza kupata umeme wa Gridi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri zaanza kupata umeme wa Gridi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mkuranga-kibiti-ikwiriri-zaanza-kupata.html
0 Response to "Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri zaanza kupata umeme wa Gridi"
Post a Comment