Loading...
title : MNEC IDDI AFANIKISHA HARAMBEE UJENZI MADARASA KANISA LA AIC KALANGALALA
link : MNEC IDDI AFANIKISHA HARAMBEE UJENZI MADARASA KANISA LA AIC KALANGALALA
MNEC IDDI AFANIKISHA HARAMBEE UJENZI MADARASA KANISA LA AIC KALANGALALA
Na,Joel Maduka,Geita.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani Geita Iddi Kassim Iddi,amefanikisha upatikanaji wa kiasi cha shilingi milioni 13.2 ,mifuko ya seruji 70 na mabanti ya kisasa 131 kwaajili ya ujenzi wa madarasa ya watoto kwenye kanisa la AIC Kalangalala Wilayani Geita.
MNEC wa mkoa huo Iddi ameendesha harambee hiyo siku ya leo kwenye ibada ambayo ilikuwa imeandaliwa na idara ya wanawake wa kanisa la AIC Kalangalala kwaajili ya changizo la umaliziaji wa madarasa ya kujifunzia watoto kanisani hapo.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya watoto wa kanisa hilo,Bi Justina Yuda ameeleza mahitaji ya ujenzi wa madarasa ya watoto kwa awamu ya pili yanatarajia kugharimu kiasi cha Tsh 19,185,000 na kwamba fedha hiyo itasaidia kuezeka,kuweka dali kwenye madarasa pamoja na kuweka frame za madirisha ,milango na mageti ya milango.
Katika harambee hiyo MNEC Iddi milioni 1 papo hapo,mifuko 20 ya seruji na mabati 13 huku akitumia nafasi hiyo kuendesha harambee ambayo iliweza kusaidia kupatikana kiasi cha sh,milioni 12.2 hivyo kupelekea kupatikana kwa jumla ya kiasi cha sh,milioni 13.2 ambazo zitatumika kujenga madarasa ya kujifunzi watoto.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Mkoani Geita Iddi Kassim Iddi,akiendesha Harambee ya umaliziaji wa ujenzi wa madarasa kwenye kanisa la AIC Kalangalala.
Mch,John Masanyiwa akisoma kiasi ambacho kimepatikana kwenye harambee hiyo ya kanisa.
Madarasa ambayo yamejengwa kwaajili ya watoto wa kanisa la AIC Kalangalala.
Mgeni Rasmi pamoja na mchungaji na viongozi wa kanisa la AIC Kalangalala wakikagua baadhi ya majengo ambayo yamekwishakujengwa.
Hivyo makala MNEC IDDI AFANIKISHA HARAMBEE UJENZI MADARASA KANISA LA AIC KALANGALALA
yaani makala yote MNEC IDDI AFANIKISHA HARAMBEE UJENZI MADARASA KANISA LA AIC KALANGALALA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MNEC IDDI AFANIKISHA HARAMBEE UJENZI MADARASA KANISA LA AIC KALANGALALA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mnec-iddi-afanikisha-harambee-ujenzi.html
0 Response to "MNEC IDDI AFANIKISHA HARAMBEE UJENZI MADARASA KANISA LA AIC KALANGALALA"
Post a Comment