Loading...
title : DC MJEMA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILALA, AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHALI YA MAFURIKO.
link : DC MJEMA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILALA, AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHALI YA MAFURIKO.
DC MJEMA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILALA, AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHALI YA MAFURIKO.
Na. John LuhendeMwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuchukua tahadhali katika kipindi hiki cha mvua nyingi ili kujiepusha na maafa ambayo ya naweza kuepukika.
Mhe. Mjema Ameyasema hayo wakati wa ziara yake akiwa ameambatana na Kamati ya usalama na Maafa ya Wilaya, katika kutembelea maeneo yaliyo atharika na mvua zinazoendelea kunyesha, huku akiwa taka wazazi kuwa karibu na watoto wao na kutowaachia kuchezea maji ya mvua.
"Wananchi angalieni Sana Kuna maeneo mengine sisalama nimeona wengine mnakusanyika maeneo hatari wengine chini ni ya nyaraka za umeme mkubwa na huku mnaongea na simu ni hatari" alisema
Aidha amewataka wakazi wa mabondeni kuhama kuepuka mafuriko kwakuwa mvua bado zina endelea kunyesha.
"Natoa pole kwa wananchi wote ambao nyumba zao zimesombwa na Mafuriko na wengine ambao nyumba zenu zimejaa maji serikali yenu iko nanyi." alisema Mjema
Kwa upande wa miundo mbinu iliyo jaa maji Mjema amewataka madereva kuwa waangarifu na barabara hizo na kufuata maelekezo kuacha kupita barabara ambazo zimefungwa hadi hapo zitakazo funguliwa.
"Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani imefungwa, na ile ya kupita club ya Yanga nayo pia imefungwa" alisema Mjema
Pamoja na hayo Mema amesema Serikali itaendelea kuboresha na kukarabati miundo mbinu iliyo haribiwa na mvua pindi mvua zitakapo Tulia kunyesha.
Kwa upande wao wananchi walio atharika na mvua wameiomba serikali kujenga mifereji na madaraka madhubuti itakayohimili maji ya mvua.
Baadhi ya maeneo alivyotembelea ni Kwamnyamani, Vingunguti, Uongozi, Ana B, ambapo kodi madarasa mawili yamesemwa na Maji, Pugu, Majohe Bangolo naMongo la Ndege
Hivyo makala DC MJEMA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILALA, AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHALI YA MAFURIKO.
yaani makala yote DC MJEMA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILALA, AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHALI YA MAFURIKO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILALA, AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHALI YA MAFURIKO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/dc-mjema-atembelea-maeneo.html
0 Response to "DC MJEMA ATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MVUA ILALA, AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHALI YA MAFURIKO."
Post a Comment