Loading...
title : KUFUNGWA KWA CHOO STENDI YA BAGAMOYO KWASABABISHA KERO KWA WATUMIAJI, HALMASHAURI YAAHIDI KUKIFANYIA KAZI BAADA YA MVUA
link : KUFUNGWA KWA CHOO STENDI YA BAGAMOYO KWASABABISHA KERO KWA WATUMIAJI, HALMASHAURI YAAHIDI KUKIFANYIA KAZI BAADA YA MVUA
KUFUNGWA KWA CHOO STENDI YA BAGAMOYO KWASABABISHA KERO KWA WATUMIAJI, HALMASHAURI YAAHIDI KUKIFANYIA KAZI BAADA YA MVUA
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
Baadhi ya watumiaji wa choo cha stendi ya Bagamoyo ,mkoani Pwani wameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuharakisha mchakato wa ukarabati wa choo hicho ambacho hakitumiki kwa takriban wiki tatu sasa.
Choo hicho kimefungwa na halmashauri hiyo baada ya kufurika maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo watumiaji wanahofia magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosa huduma hiyo na kusababisha baadhi ya watu kujisaidia kiholela.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye stendi hiyo watumiaji hao wakiwemo wasafiri,madereva na mama lishe walisema kukosekana kwa huduma hiyo ni hatari kwa afya za wananchi. Agnes Robert ambaye ni mama lishe kwenye stendi hiyo alisema kukosekana kwa huduma hiyo ni changamoto kubwa kwao na kwa wateja wao wanaopata huduma kwenye migahawa yao.
"Tunapata shida kwa wateja wetu ambao wengi ni abiria wakishuka kwenye mabasi huhitaji huduma ya choo kabla ya kupata riziki ya chakula. Tunapowaambia hakuna choo wanalalamika sana hivyo tunaiomba halmashauri iangalie namna ya kufanya ukarabati kwa haraka" alisema Agnes.
Dereva wa mabasi yanayofanya safari Kiwangwa ,Fikiri Mohammed alieleza kutokana na vyoo kufungwa baadhi ya watu wamekuwa wakijisaidia kiholela kwenye eneo la stendi. Alisema kwamba ,wanahofia hali hiyo inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko. "Uchafu na maji ya chooni yanazagaa hii ni hatari kwa watu wanaotumia stendi ,choo bora ni kitu muhimu sana hapa kwa afya zetu" alisema Mohammed.
Akijibu malamiko hayo, mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu alisema changamoto hiyo imetokana na eneo hilo kuwa na chemchem inayotoa maji na kufanya eneo hilo kujaa maji.Alielezea ,tayari wameshafanya uchunguzi na kuangalia sehemu nyingine ya eneo pembeni kwa ajili ya kuchimba shimo lingine ambalo halitapitisha maji.
Kwa mujibu wa Latu ,wanaendelea na mchakato na wanatarajia kutumia zaidi ya milioni tatu (3), kwa ajili ya shimo hilo ambapo fedha zitatokana na mapato ya ndani.Latu alisema ,ujenzi huo utaanza kufanyika mara baada ya mvua zinazoendelea kunyesha zitakapo kwisha kwani kwa sasa ujenzi hautaweza kufanyika.
Hivyo makala KUFUNGWA KWA CHOO STENDI YA BAGAMOYO KWASABABISHA KERO KWA WATUMIAJI, HALMASHAURI YAAHIDI KUKIFANYIA KAZI BAADA YA MVUA
yaani makala yote KUFUNGWA KWA CHOO STENDI YA BAGAMOYO KWASABABISHA KERO KWA WATUMIAJI, HALMASHAURI YAAHIDI KUKIFANYIA KAZI BAADA YA MVUA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUFUNGWA KWA CHOO STENDI YA BAGAMOYO KWASABABISHA KERO KWA WATUMIAJI, HALMASHAURI YAAHIDI KUKIFANYIA KAZI BAADA YA MVUA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/kufungwa-kwa-choo-stendi-ya-bagamoyo.html
0 Response to "KUFUNGWA KWA CHOO STENDI YA BAGAMOYO KWASABABISHA KERO KWA WATUMIAJI, HALMASHAURI YAAHIDI KUKIFANYIA KAZI BAADA YA MVUA"
Post a Comment