Loading...
title : Michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kutumika kuibua vipaji vya wanamichezo nchini
link : Michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kutumika kuibua vipaji vya wanamichezo nchini
Michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kutumika kuibua vipaji vya wanamichezo nchini
Na Genofeva Matemu – WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka walimu wa michezo nchini kutumia michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kuibua vipaji kupitia hazina ya vijana wadogo waliopo katika shule za msingi na sekondari wenye uwezo mkubwa katika michezo mbalimbali.
Rai hiyo ameitoa Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao na wadau wa sekta ya michezo kujadili namna ambavyo michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA itakavyoendesha mwaka huu ambapo michezo hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia mwezi Juni mwaka huu Jijini Mwanza.
“Tumedhamira kuibua vipaji kuanzia ngazi ya shule za msingi ili tuweze kuliweka taifa katika taswira ya michezo kwani michezo ni sayansi inayohitaji mazoesi yanayoweza kuisaidia jamii kuwa na afya bora na hata kuweza kuitangaza nchi katika mataifa mengine kupitia michezo mbalimbali” amesema Mhe. Mwakyembe.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amewataka wadau wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi kuchangia ili kufanikisha michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA na kuifanya michezo hiyo kuwa agenda kubwa hapa nchini katika kuendeleza michezo na kuinua vipaji vya michezo mbalimbali.
Aidha Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Dkt. Yahya Msigwa amesema kuwa Michezo ni kila kitu katika jamii kwani michezo ni ajira, michezo ni siasa, michezo ni kinga dhidi ya ukimwi na kinga dhidi ya ujambazi kwa vijana, michezo ni biashara, michezo ni utamaduni na pia michezo haina mipaka kati ya nchi na nchi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi na wadau kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifafanua jambo wakati wa kikao cha maandalizi na wadau kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Elimu Bw. Tixon Nzunda
Baadhi ya wadau wa sekta ya michezo wakifuatilia hoja wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Maganga Japhet akichangia mada wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia waliokaa) pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(wapili kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa michezo walioshiriki katika kikao cha maandalizi kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu - WHUSM
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kutumika kuibua vipaji vya wanamichezo nchini
yaani makala yote Michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kutumika kuibua vipaji vya wanamichezo nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kutumika kuibua vipaji vya wanamichezo nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/michezo-ya-umisseta-na-umitashumta.html
0 Response to "Michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kutumika kuibua vipaji vya wanamichezo nchini"
Post a Comment